aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, November 30, 2013

Ni Tshs. 20,000/= tu Kushuhudia Fainali za Bongo Star Search (BSS) hapo Kesho J'mosi Nov 30, 2013

 
Najua Watanzania wameshuhudia foleni kubwa sana ya Bongo star search 2013 kupitia TV, Magazeti na hata kusikia kwenye Radio kuhusu waliojitokeza kushiriki ila mshindi ni mmoja na atajulikana Jumamosi November 30 2013 kwenye fainali ambazo nimeambiwa zinafanyika ufukweni, sehemu inayovutia na salama kabisa kwa kila mtu.

Nimeambiwa pia Mshindi anajichukulia milioni 50 ambapo  waliofanikiwa kuingia fainali ni Amina Chibaba (MBEYA), Melisa John (DSM), Elizabeth Mwakijambile (DSM), Emmanuel Msuya (MWANZA) na Maina Thadei (DSM) ambapo kabla ya mshindi kutangazwa,  Snura, Barnaba, Young Killer, Shaa, Walter Chilambo, Peter Msechu  na Makomandoo watapewa nafasi ya kumiliki stage.

VIP unaimiliki kwa  50,000/ na huku kwingine ni 20,000/=ambapo  tiketi  za siku ya Fainali zinapatikana Shear illusion,  Biggy Respect (Kariakoo) Steers Mjini, Zizzou Fashion (Victoria na Sinza) Photo Point (Mayfair) Robby One Fashion (Kinondoni)  Best Bite, Engen Mbezi,   Escape One (Mikocheni), Benchmark Office Mikocheni,  American Nails (Kinondoni).

No comments:

Post a Comment