aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, November 29, 2013

Kada wa CCM Zanzibar Acharangwa Mapanga kama Mdudu wakati akitoka harusini Nyakati za Usiku..!!


Kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM Jimbo la Mpendae, Hassan Abdallah Said (25) ameshambuliwa kwa mapanga wakati akitoka harusini saa tano usiku.
Akizungumza na Mwananchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Khamis Mkadam alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema maafisa wa upelelezi wameanza kufanya uchunguzi.
Makadam alisema uchunguzi wa awali umemwonyesha kuwa kijana huyo alishambuliwa na watu wasiojulikana kabla ya kupelekwa Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa matibabu .

 “Ni kweli tukio hilo limetokea, tumeanza kufanya uchunguzi ikiwemo kutafuta taarifa muhimu zitakazosaidia uchunguzi wetu kufanikiwa kuanzia katika eneo la tukio na kuhakikisha waliofanya uhalifu huo wanakamatwa,” alisema Mkadam
Hata hivyo Mkadam alisema ni mapema kuzungumzia chanzo cha tukio hilo na kuwataka raia wema kuwasaidia kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu.Akizungumza kwa shida huku akiwa hospitali, majeruhi Hassan alisema alikuwa akitoka kwenye sherehe ya harusi na kuitwa na watu wawili akitakiwa asimame.
“Niliitwa na kufikiri kama ni utani, waliniita wee CCM mjinga hebu simama, nikasimama na ghafla wakaongezeka wengine na kuanza kunishambulia kwa mapanga,” anaeleza Hassan. Hassan alieleza kuwa shambulio hilo ni la kisiasa na kwamba anawafahamu vijana wawili waliokuwa wakishiriki harakati za Jumuiya ya Uamsho.

No comments:

Post a Comment