aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, November 17, 2013

AFANDE SELE ATOA YA MOYONI KUHUSU BABU SEYA NA PAPI KOCHA

Huwa nawakumbuka naamini kabisa kitambo si kirefu watakua huru.. wakati nafanya album yangu ya kwanza (mkuki moyoni) zaidi ya miaka kumi iliyopita kuna ile track MAYOWE REMIX imepigwa live band ingawa MAJANI alipiga kick, lakini BASE & SOLO GUITAR alicharaza MZEE NGUZA (babu seya) mwenyewe, ukisikiliza vyema ile kazi utasikia kila chombo kwa wakati wake hiyo imechangiwa na ustadi wa Mzee Nguza zaidi, mtoto wake ambae ni PAPII KOCHA alifanya chorus ilikua vibe sana nakumbuka siku ile pale BONGO RECORDS. wakati huu ambao nakaribia kutimiza miako kumi ya KING OF RHYMES i wish mungekuepo tufanye kitu, MFUNGWA, MFUNGWA NI NANI? IMAM, RAISI. ASKOFU, MWALIMU, HAKIMU, JAJI, MASIKIN, TAJIRI, MCHUNGAJI anaweza kuwa mfungwa... .. MUNGU ni muweza wa yote na hashindwi na chochote naamini kabisa tutakua pamoja uraiani .. nawapenda, nawaombea na maelfu ya Watanzania wako pamoja nanyi

No comments:

Post a Comment