aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, November 21, 2013

Hiki Ndicho kilichomsibu Msanii BERRY WHITE alipochoma moto Gari ya demu wake baada ya kuhisi kuwa Anasalitiwa Penzini..!!

Msanii Berry White


Berry ambaye jina lake halisi ni Mbaraka, alikuwa akimtuhumu mchumba wake kuwa anamsaliti. Kufuatia tukio hilo, msanii huyo anashikiliwa na polisi kwenye kituo cha Osyterbay jijini Dar.

Akiongea na Gossip Cop kwenye You Heard ya Clouds FM leo, baba mzazi wa msanii huyo aishiye Zanzibar amesema wanafanya kila jitihada wamtoe msanii huyo.
Tumepanga kuongea na huyu anayeishi naye tukae kitako kwa upande wangu mimi ntaweza kumfidia tu gari. Wao tunapenda tu wasikilizane, na tuko tayari kukaa kitako na mwanamke kumnunulia gari,” amesema Mzee huyo.


Hata hivyo amekanusha taarifa kuwa mwanae amekuwa akifanya matukio mengi ya kihalifu kwa mchumba wake huyo ikiwa ni pamoja na kuuza vitu vyake na kumpiga mara kwa mara. Hapana uhalifu mjomba, mimi niko nao hawa ana kwa ana huyu Sayla na huyu Mbaraka mwanangu. Ni mambo ya kike kike na ya kiume kiume tu wanafanya matatizo hapa na pale, sio matatizo makubwa kama hayo niliyosikia.


Mzee huyo ambaye huishi Oman na aliyekuja kwenye msiba wa mwanae mwingine visiwani Zanzibar, ameongeza kuwa yeye ameshindwa kuja Dar es Salaam kushughulikia suala hilo kutokana na kuwa mgonjwa lakini mkewe, wanae na dada zake na ndugu zake wengine wamekuja.


Alisema mwanae na mchumba wake nao walikuwepo kwenye msiba wa mwanae mwingine huko Zanzibar na walikuwa wakilala chumba kimoja na baba yao na hawakuwa na tatizo lolote. “Hivi juzi walikuwa pamoja mazikoni hapa walikuwa wanalala chumba kimoja na mimi, yeye huyo mke na mwanaume mtoto wangu, mimi nimelala juu ya kitanda wao magodoro chini wamelala.


Alimalizia kwa kudai kuwa pindi mambo hayo yakiisha, yupo tayari kuwaozesha wawili hao waishi kihalali kama mke na mume.


SIKILIZA U HEARD HAPA 

No comments:

Post a Comment