aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, November 21, 2013

UKATILI: Hivi ndivyo jinsi Kikongwe Alivyouawa kikatili kwa kuchunwa Ngozi huko Morogoro

Tukio la kifo cha kikongwe, Hellan Petri Mahunzila (75) ambaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha kwa siku 12 kisha siku ya 13 mwili wake kuonekana kando ya shamba lake huku  mwili wake ukiwa imechunwa ngozi mwili mzima, imezua hofu kubwa. 
Familia iliyohusika kumsaka kikongwe Helena Petri siku aliyopotea.Picha na Juma Mtanda 

  

Wakazi Kitongoji cha Gongo, Kijiji cha Mgata, Kata ya Bwakilajuu mkoani Morogoro, ambako tukio hilo limetokea, sasa wanaishi kwa hofu.
Baadhi yao  wanalazimika kujisaidia haja ndogo na kubwa katika makopo hasa nyakati za usiku, ndani ya nyumba zao. Tukio hilo limebadili kabisa mfumo wa maisha na kutembea, wengi wanalazimika kuingia ndani ya nyumba kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12:30 jioni wakihofia kutekwa.
Tukio lenyewe
Ni  saa 7 usiku, siku ya Jumatano kuamkia Alhamisi ya Oktoba 2 mwaka huu, Eliza Steven (19) anaamka na kumnyonyesha kichanga chake,  James Peter (miezi mitatu), baada ya kilio cha mtoto huyo mchanga kuhitaji kunyonya.
Baada ya James kunyonya na kushiba, alinyamaza kulia, hiyo ilikuwa ni kama kumpa fursa mama yake kutoka ndani ili aende nje kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo.
Anafungua mlango wa chumba chake na kutoka nje kujisaidia huku akipiga jicho na kuangalia mlango wa chumba anacholala bibi yake,  anaona mlango upo wazi. Jambo hilo, hakulitilia shaka sana kwani alikuwa na imani angeweza kukutana naye nje ama chooni,  haikuwa hivyo.
Alilazimika baadaye kuingia  chumba anacholala bibi huyo, aliangalia kitandani ili kuweza kujibu maswali yake yaliyojaa kichwani likiwamo la kwa nini bibi yake ameshindwa kufunga mlango kama alitoka nje? Anaanza kusema Eliza. Eliza aliendelea kueleza kuwa baada ya kuchunguza katika chumba kile kinachotumiwa na bibi yake, Hellen ambaye alikuwa na kawaida ya kufunga mlango pindi aiingiapo kulala, hakumwona na kuchukua jukumu la kumwamsha mama yake mzazi, Yustina Kasian (40) ili aweze kusaidiana naye kumtafuta.
Yustina Kasian ambaye ni mtoto wa pili kwa kuzaliwa kwa bibi, Hellen Petri Mahunzila anasema baada ya kuelezwa maneno yale na mtoto wake, Eliza Steven ambaye ni bibi yake alienda katika kile chumba anacholala mama yake na kuangalia huku na huku, bila mafanikio.
“Nilienda chooni na kuangalia ndani ya choo lakini sikumwona, nilirudi ndani na kumwamsha mume wangu, Steven Francis (50) ili naye atusaidie kumfuata kwani tayari hofu ilianza kutanda moyoni mwetu na kujiuliza maswali ambayo hatukuweza kupata majibu usiku ule,” anasema Yustina.
Mimi baada ya kuelezwa jambo hilo na mke wangu nilitoka nje na tochi hadi chooni na kumulika ndani na kuzunguka kile choo, sikuweza kumwona. Nilienda pia kumtafuta  kwenye banda la kupikia na eneo zima la migomba lakini mama mkwe wangu hakuweza kuonekana akiwa hai ama amekufa,” anasema Steven Francis.
Francis anasema baada ya kushindwa walikwenda kwa majirani kuomba msaada wa kumtafuta; walikwenda kwa jirani Selis Silili na Calist Stephano.

No comments:

Post a Comment