Ruth Suka ‘Mainda’. |
Vincent Kigosi ‘Ray' |
Chuchu Hans. |
Mbali na Mainda kutoboa uhusiano wake wa kimapenzi na Ray, pia aliweka wazi jinsi wasanii wenzake, Blandina Chagula ‘Johari na Chuchu Hans, walivyomuingilia kwenye penzi lake hilo.
Blandina Chagula ‘Johari’
|
Aidha, msanii huyo ambaye pia hupenda kujiita Small Baby aliliponda kundi la Bongo Movie Unit kwa kusema kuwa limejaa uchafu.
Risasi Mchanganyiko liliwasaka Ray, Johari na Chuhu ili kuweza kupata mzani wa habari kuhusiana na kile alichokiongea Mainda lakini wasanii hao wamekuwa wakiogopa kusema chochote.
Katika hali ya kuonesha kumhofia Mainda, Ray amekacha miadi na mwandishi wetu mara kadhaa.
Naye Johari amekuwa akisema kwamba Mainda amewavua nguo huku akikataa kufunguka zaidi.
Kwa upande wake, Chuchu amekuwa akigoma hata kupokea simu za waandishi wetu.
Gazeti hili lilipomtafuta Mainda alisema hakuna kitu anachokiogopa chini ya jua.
“Kwanza sioni kibaya nilichokiongea, bado nina mambo mengi zaidi ya hayo,” alisema staa huyo na kuongeza kwamba hakuna mtu wa kumziba mdomo.
“Ninachoweza kuwaambia ni kwamba niko tayari kufia kwenye mapambano, sitaogopa chochote,” alisema Mainda.
----GPL
No comments:
Post a Comment