Saturday, November 23, 2013
Nesi Mkoani Dodoma Aingia matatani kwa kashfa ya Kung'oa Nywele za sehemu za siri(NYETI) za wajawazito kikatili kwa kutumia Kucha za mikono badala ya Kiwembe..!!
MUUGUZI wa Zahanati ya Kata ya Mondo, Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, aliyetajwa kwa jina la Laurensia Nombo, ameingia katika kashfa, akidaiwa kuwafanyia vitendo vya kikatili wajawazito. Taarifa zilizolifikia RAI Jumamosi zimeeleza kuwa muuguzi huyo amekuwa akilalamikiwa kutokana na tabia yake ya kuwadhalilisha wagonjwa, hususan wanawake.
Wananchi waliozungumza na gazeti hili bila kutaka majina yao kutajwa gazetini, walisema muuguzi huyo maarufu kwa jina la Mcharuko, amekuwa akitoa lugha chafu kwa wagonjwa na kufanya kazi kwa vitisho.
Wananchi hao walisema muuguzi huyo amekuwa akiwaumiza wajawazito kwa kuwanyonyoa nywele sehemu zao za siri kwa mkono kwa kisingizio cha usafi, kitendo ambacho huwasababishia maumivu makali.
“Huyu nesi hana lugha nzuri kwa wagonjwa, anawatisha, kibaya zaidi anawadhalilisha akina mama wajawazito wanapokwenda kiliniki kupata huduma au kujifungua.
“Anawavuta nywele sehemu zao za siri, kama ni usafi kwanini asitumie kiwembe au mkasi, badala yake anawavuta nywele kwa mkono. Hii ni huduma au ukatili?
“Huyu nesi anafanya biashara ya nguo za ndani, huwa anawachania nguo za ndani akina mama akijifanya anakagua, lakini lengo la ni kufanya biashara. Sisi ni wanaume, tumechoshwa na ukatili wanaofanyiwa wake zetu na dada zetu pale zahanati,” alisema mwananchi huyo.
Wananchi hao walidai kuwa muuguzi huyo amekuwa akilindwa na baadhi ya viongozi wa kata, huku wakipinga mpango unaoandaliwa wa kuhamishwa muuguzi mwingine aliyetajwa kwa jina la Anna Eusebi.
“Pale kuna nesi mwingine anaitwa Anna, huyu alihamishiwa hapa akitokea Goima, ni nesi mzuri anatoa huduma nzuri na wananchi wanampenda, lakini amefanyiwa majungu wanataka kumhamisha,” alisema.
Mwananchi mwingine alisema wananchi wa kata hiyo hawatakubali kuona muuguzi huyo mzuri anahamishwa na kuachiwa muuguzi muovu ambaye analalamikiwa.
“Tumesikia muda wowote huyu nesi mzuri atahamishwa, tumejipanga kumlinda, tunasubiri hilo gari la halmashauri lije, hatutakubali tutakwenda kuzuia gari pale. Mkuu wa wilaya hafanyi mikutano na wananchi, asikilize kero zetu, yeye akija anafanya mikutano ya ndani na viongozi tu,” alisema.
Kwa mujibu wa wananchi hao, Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Francis Isack, amefuta barua ya uhamisho wa muuguzi anayelalamikiwa na badala yake akaidhinisha uhamisho wa muuguzi anayependwa, jambo linalopingwa na wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment