aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, November 23, 2013

Kijana aukata uume wake kuepuka usumbufu wa wanawake huko Tabora...!!



Ayubu Mnazi Alphonce(24) ni  kijana  ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete akipatiwa matibabu baada ya kuamua kuukata uume wake kwa  kutumia  wembe  mpya  ili  kuepukana  na  usumbufu anaoupata kutoka kwa wanawake ambao amekuwa nao  kimapenzi...
Imeelezwa kuwa baada ya kutokea mfarakano baina yake na mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika,Ayoub  aliamua kuingia ndani na kuukata uume wake kwa kutumia wembe mkali na kisha kuutupa  nje..



Taarifa kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa baba mzazi wa Ayubu baada ya kubaini kuwa mtoto wake alikuwa  amejifungia chumbani kwa muda mrefu, aliamua kumgongea mlango na alipopata fursa ya kuingia ndani ndipo alipogundua ukweli juu ya jambo hilo na hivyo kumpeleka Ayubu Kituo kikubwa cha Polisi Tabora ambapo jalada la kesi ya kujidhuru lilifunguliwa.



Hata hivyo hali ya Ayubu kwasasa inaendelea vizuri licha ya kuwa amejikata na kubakisha kipande cha sentimeta 5 huku akisubiriwa kufikishwa mahakamani kwa kutenda kosa hilo la kujidhuru mwenyewe pasipo sababu za msingi.


No comments:

Post a Comment