aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Sunday, October 27, 2013

NEWZ ALERT: BABA MZAZI WA WEMA SEPETU AFARIKI DUNIA....!!



Taarifa  tulizozipata  zinaarifu  kuwa Balozi Isaac Abraham Sepetu   ambaye  ni  baba  mzazi  wa  Wema  Sepetu ameaga dunia.

Balozi Sepetu alikuwa amelazwa kwa miezi kadhaa hospitalini jijini Dar es Salaam  kwa maradhi ya kiharusi na kisukari  na  mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar.

Balozi Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Kambarag Nyerere. 

Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere. Machi 27, mwaka huu, Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais wa Zanzibar, Dk Mohammed Shein,  kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega uchumi ya Zanzibar (ZIPA).

 
 

Mungu  ailaze  roho  ya  marehemu  mahali  pema  peponi-Amina.

No comments:

Post a Comment