aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, October 23, 2013

KANISA LAVAMIWA JIJINI MWANZA NA WATU WASIOJULIKANA,MMOJA AUAWA NA WENGINE WAWILI WAJERUHIWA VIBAYA....


 
Wananchi wakiwa wakitafakari nje ya jengo la Kanisa la Gilgal Christian Centre lililopo Pasiansi Ilemela jijini Mwanza.
 ----------
Mtu mmoja ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia shambulizi lililofanywa na kundi la watu wasiofahamika usiku wa kuamkia jana  katika kanisa la Gilgal Christian Worship Centre lililopo eneo la Pasiansi wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.

Tukio hilo lililotokea majira ya saa saba usiku linamtaja Elia Lunyamila (35) ambaye ni mlinzi  na ni  mwenyekiti wa vijana wa kanisa kuuawa akiwa amejumuika kwenye ibada na waumini wengine Alex Msakuzi na Tumsifu Pungu ambao hali zao zinatajwa kuwa taabani wakipatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kukatwakatwa mapanga sehemu mbalimbali za miili  yao. 

Askofu wa kanisa hilo Eliabu Sentoz amelaani tukio hilo akilitaja kuwa ni la kinyama kwani limefanyika sehemu ya ibada akiwataka wananchi kuungana pamoja kulisaidia jeshi la polisi katika kutoa taarifa kuwabaini wahusika wa shambulio  hilo na akaiomba serikali kuongeza nguvu kukabiriana na wahalifu hao.


Kamanda wa polisi mkoa wa  Mwanza , Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo mpaka sasa hakuna taarifa za kuibiwa kwa kitu chochote ndani ya kanisa, hali ambayo inalifanya tukio hilo kuwa na maswali mengi likihofiwa kufananishwa na yale ya uchomaji moto Makanisa.
Waumini wakitafakari tukio hilo la uvamizi lililosababisha taharuki  kwa wakazi wa jiji la Mwanza.
 
 
Ndugu na majirani pamoja na waumini waliomfahamu marehemu Elia Lunyamila aliyeuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu kuomboleza 
 Askofu wa kanisa la Gilgal Christian Centre Eliabu Sentozi.
 

No comments:

Post a Comment