aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, October 30, 2013

MTOTO WA DARASA LA SITA APOOZA MIGUU MARA BAADA YA KUCHAPWA FIMBO NA MWALIMU WAKE KWA KOSA LA KUNYWA MAJI YA SHULE BILA RUHUSA..!!

MWANAFUNZI wa darasa la sita, Ismail Godfrey (13) anayesoma katika Shule ya Msingi Maendeleo  Sinuka iliyopo mkoani Kigoma amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kudai  kutandikwa viboko  na Mwalimu Muige Joseph na kupooza miguu. 
 
Mtoto Ismail Godfrey akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar.
Mtoto huyo ambaye kwa sasa anapata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar baada ya kukosa matibabu ya kina mkoani Kigoma alipokutana na mwandishi wetu alikuwa na haya ya kusema:
“Awali sikuwa na matatizo yoyote ya kiafya hususan katika viungo vya mwili, isipokuwa haya yalinipata baada ya kuchapwa fimbo na mwalimu wangu ndipo nikapooza ghafla.

Miguu ya mtoto Ismail iliyopooza.
Tukio hili lilitokea mwezi wa tano nilipokuwa shuleni, nilipofika nilifungua bomba nikawa nakunywa maji kwa kuwa nilikuwa na kiu, ghafla mwalimu huyo alikuja na kuniambia kwa nini nachezea boma,  ndipo akaanza kunitandika viboko. Hapo hapo nikahisi viungo vyote vya mwili vimepoa na miguu ikapata ganzi, nikaanguka chini baada ya kukosa nguvu,” alisema Ismail.
 Kutokana na tukio hilo baba wa mtoto huyo,  Godfrey Lucas aliitwa  na baada ya kuona Ismail yupo katika  hali hiyo ya kupooza miguu aliamua kumpeleka katika Hospitali ya Mkoa, Maweni, kupatiwa matibabu, huku akifanya juhudi za kumtafuta mtuhumiwa ambaye alikuwa amekimbia makazi  yake.

Ismail Godfrey.
Hata hivyo , kutokana na juhudi za kumtafuta kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kumkamata mwalimu huyo katikati ya mji wa Kigoma na kumfikisha polisi ambapo alifunguliwa kesi kwa jalada namba  KIGO/RB/2269/013 17/3/2013 SHAMBULIO LA MWILI.
 Mtoto alianza kutokwa na vidonda miguuni ndipo nikaamua tuje hapa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na tukapokelewa na mtoto amelazwa wodi ya wagonjwa ya Kibasila,” alisema. 
 Hata hivyo, amesikitika kuachiwa mtuhumiwa kwa dhamana wakati  mwanaye bado kalazwa na anakosa masomo kwa sababu yake.

No comments:

Post a Comment