Mwigizaji staa wa Nollywood, Jim Ikye amefunguliwa kutoka katikavifungo vya roho za shetani kwenye kanisa la T.B Joshua huko Nigeria jumapili, Septemba 29 kwenye show ya ukombozi inayoonyeshwa live na Emmanuel TV.
Roho hizo za kishetani zilikuwa zinamzuia yeye kupata mchumba wa kumuoa. Alivamiwa na mashetani hayo n kuanza kuconfess. Roho hizo ziliongea kupitia yeye na kusema kuwa hizo roho zilikuwa ndo sababu ya kutoendelea kwake na kumkatisha tamaa na kwamba ni neema ya Mungu tu pekee ndio iliyomfanya awepo.Mchungaji akasema ameokolewa kutoka kwenye roho hizo zilizokuwa zimemfung asioe.
Lakini staa huyo alipofunguliwa na kurudi katika hali yake ya kawaida,kitu cha kwanza alichowauliza mashemasi kilikuwa ‘Where are my shoes meen’ (viatu vyangu viko wapi meen).
No comments:
Post a Comment