Saturday, November 30, 2013
Wananchi wa jiji la Arusha ambao ni wafuasi wa CHADEMA waandamana na mabango wakimshinikiza Godbless Lema ajiuzulu kwa kuwa jimbo limemshinda
Wafuasi wa CHADEMA jijini Arusha walioambatana na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Monduli Bw. Amani Salenga wakionyesha bango hilo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani)..
Amani Salenga akiwa na kundi kubwa la vijana walikutana na waandishi wa habari na kudai kuwa Mbunge wa Arusha, Godbless Lema ndo chanzo cha vurugu ndani ya CHADEMA kwa kuanzisha kikundi cha vijana kinachohatarisha maisha ya wale wanaopinga na mawazo ya Lema katika utendaji wa chama mkoani Arusha.
Amani alisisitiza kuwa kwa kuwa CHADEMA imeamua kufanya maamuzi kwa maslahi ya watu binafsi hususani swala la viongozi waliovuuliwa vyeo vyao(zitto),basi kila mwanachadema anatakiwa atambue kuwa ndani ya chama hicho kuna pande mbili , CHADEMA ASILI na CHADEMA FAMILY.
Vijana hao waliokuwa na mabango mbalimbali wamelaani hatua ya chama chao kuwafukuza viongozi wao pasipokufuata katiba ya chama na kusisitiza kuwa Lema ndo tatizo ndani ya Chadema .
Amani alisisitiza kuwa kwa kuwa CHADEMA imeamua kufanya maamuzi kwa maslahi ya watu binafsi hususani swala la viongozi waliovuuliwa vyeo vyao(zitto),basi kila mwanachadema anatakiwa atambue kuwa ndani ya chama hicho kuna pande mbili , CHADEMA ASILI na CHADEMA FAMILY.
Vijana hao waliokuwa na mabango mbalimbali wamelaani hatua ya chama chao kuwafukuza viongozi wao pasipokufuata katiba ya chama na kusisitiza kuwa Lema ndo tatizo ndani ya Chadema .
MWANA FA,AY NA HERMY B WAMALIZA BIFU..!!
‘Friends again’, ni maneno yaliyoandikwa na Amani Joachim (Chief Operations Officers wa B’Hits), kwenye ukurasa wake wa facebook na kupost link yenye picha inayowaonesha AY, Mwana FA, na Hermy B wakiwa kwenye picha moja.
Wengine kwenye picha hiyo ni Fid Q, Carol Ndosi na Arthur.
Picha hiyo imepigwa usiku wa kuamkia leo (November 29) inamuonesha Producer wa ‘Habari Ndiyo Hiyo’ Hermy B baada ya kumwagia ndoo ya maji katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Leo mchana Hermy B amepost picha akiwa na FA uwanja wa ndege wa J.K na kuandika ‘Bday continues’.
MWANAFUNZI ATEKWA HUKO MOSHI NA KUBAKWA KWA MUDA WA SIKU NNE....!!
MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Marangu inayomilikiwa na kanisa Katoliki jimbo la Moshi, (jina limehifadhiwa) alitekwa na kukufungiwa kwenye hoteli moja ya kitalii mjini hapa na kufanyiwa vitendo vya ngono kwa muda wa siku nne mfululizo.
Mwanafunzi huyo anadaiwa kutekwa Agosti 6 mwaka huu na kijana mmoja (jina linahifadhiwa) mfanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi (Airtel) mjini Dodoma.
Akizungumza jana na Tanzania Daima Jumatano, kaka wa mwanafunzi huyo, Joseph Temba, alidai mdogo wake alitekwa na mtu huyo na tayari mtuhumiwa ameshakamatwa.
Alisema walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Agosti 10, mwaka huu, katika baa moja akiwa na mdogo wake baada ya raia wema kutoa taarifa za kuonekana kwake.
Kwa mujibu wa kaka wa mwanfunzi huyo siku ya tukio alipokea simu kutoka kwa mwangalizi wa wanafunzi (matroni) akimjulisha kutokuwapo bwenini kwa mdogo wake na ndipo walipoanza kufuatilia na kutoa taarifa kituo kikuu cha polisi mjini Moshi na kupewa namba Mos/RB/9196/2013.
Alisema siku iliyofuata ya Agosti saba jioni walipokea simu kutoka kwa watu wa karibu wakiwataarifu kuwapo katika hoteli hiyo mdogo wake lakini baada ya kufika walinyimwa kuona kitabu cha wageni ili kuangalia orodha ya majina ya wageni waliofikia hapo ili kujiridhisha kama mtuhumiwa huyo alikuwapo mahali hapo.
Hata hivyo alisema jioni ya Agosti 10 walipokea taarifa za kuonekana kwenye baa hiyo mtuhumiwa akiwa na mdogo wake na kuwajulisha polisi na hatimaye kufanikiwa kumtia mbaroni ambapo hadi sasa bado anahojiwa na jeshi la polisi.
Chanzo cha kutekwa kwa mwanafunzi huyo ni mawasiliano ya simu baina ya mtekaji na mwanafunzi huyo ambapo inadaiwa mtuhumiwa huyo alimrubuni mwafunzi huyo kuacha masomo na kwamba angemtafutia nafasi kwenye shule kubwa za kimataifa.
Inadaiwa kwamba mwanfunzi huyo alikubaliana na propaganda hiyo na kutoka shuleni jioni ya Agosti 6 na kumfuata mtuhumiwa kwenye gari lake na kwenda naye hadi Moshi mjini umbali wa kilomteta 50 kutoka shule ya sekondari Marangu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alisema hana taarifa za kutekwa kwa mwanafunzi huyo kwa kile alichodai alikuwa ametingwa na majukumu ya kikazi mjini Arusha na kuahidi kulifuatilia baadaye
Hizi Ndio sababu za kwanini Wabunifu wengi wa mitindo wa kiume Duniani ni 'Mashoga'...!!
Bila shaka umeshajiuliza sana kwanini wabunifu wengi wa nguo wa kiume duniani ni mashoga. Haya ndio majibu:
Kwanza, tasnia ya mitindo (fashion industry) kiutamaduni imekuwa ikiwakubali zaidi mashoga wanaojulikana wazi (openly gay men) tofauti na fani zingine. Hata leo, ni changamoto kubwa kwa shoga kufikia level ya kuwa CEO ama Mkurugenzi kuliko wanaume wa kawaida.
Tofauti ni kwamba shoga kwenye fashion anaweza kuheshimika na kuenziwa kwenye fani hiyo na kufanikiwa binafsi na kifedha bila kudhihakiwa kama ambavyo anaweza kujikuta akifanyiwa kwenye fani zingine kama upolisi, jeshi na kwenye michezo.
Marc Jacobs
Mifano mizuri inaweza kuwa kwa manguli wa fashion duniani kama Valentino Garavani, Yves Saint Laurent, Perry Ellis, Karl Lagerfeld, Alexander McQueen, Gianni Versace, Alexander Wang, Giorgio Armani, Marc Jacobs (Louis Vuitton) Domenico Dolce na Stefano Gabbana, Tom Ford na wengine. Na hata kwa Tanzania wapo wengi wanaofahamika wazi.
Karl Lagerfeld
Japokuwa mambo yanabadilika na hasa kwa nchi za wenzetu na kukubalika kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, kumefanya mashoga nao wafanikiwe kwenye fani zinazotawaliwa na wanaume wa kawaida, lakini mifano ya dunia halisi inabaki michache na hasa tu kwenye majiji ama nchi ambazo mashoga na wasagaji wanapewa heshima sawa na wengine.
Pia kihistoria mashoga kwenye fashion walikuwa wakipewa kipaumbele zaidi kuliko wanawake. Ni Coco Chanel pekee ndio alikuwa miongoni mwa wanawake wachache waliofanikiwa kwenye kiwanda hicho kilichokuwa kikitawaliwa zaidi na mashoga Christian Dior na Cristobal Balenciaga.
Dolce & Gabbana
Pili, inasemekana kuwa utamaduni wa ushoga huwapa nafasi watu hao uwezo wa ubunifu. Mashujaa kwenye jumuiya ya mashoga sio wachezaji wa soka ama wanajeshi- japo wapo. Lakini zaidi wapo kwenye muziki, uigizaji, utengezaji wa filamu, uandishi na sanaa zingine.
Hii ni kwasababu ya ukweli kwamba hizi ndio zilikuwa kazi ambazo mashoga waliweza kufanikiwa na kuendelea kuwa walivyo na kujivunia wanachokifanya. Uwezo wao wa ubinifu huongezeka na ile sense ya upekee ambayo mashoga huikuza ndani ya ulimwengu wa mapenzi ya jinsia mbili (heterosexual world).
Tom Ford
Pointi ya msingi: Upenzi wa mashoga katika urembo, utanashati hauwezi kuelezeka. Inasemekana kuwa mwanaume anayebuni nguo nzuri kwa mwanamke aidha hutaka kuwa na mwanamke ama hutaka kuwa mwanamke’
Credit: Bongo 5
Kwanza, tasnia ya mitindo (fashion industry) kiutamaduni imekuwa ikiwakubali zaidi mashoga wanaojulikana wazi (openly gay men) tofauti na fani zingine. Hata leo, ni changamoto kubwa kwa shoga kufikia level ya kuwa CEO ama Mkurugenzi kuliko wanaume wa kawaida.
Tofauti ni kwamba shoga kwenye fashion anaweza kuheshimika na kuenziwa kwenye fani hiyo na kufanikiwa binafsi na kifedha bila kudhihakiwa kama ambavyo anaweza kujikuta akifanyiwa kwenye fani zingine kama upolisi, jeshi na kwenye michezo.
Marc Jacobs
Mifano mizuri inaweza kuwa kwa manguli wa fashion duniani kama Valentino Garavani, Yves Saint Laurent, Perry Ellis, Karl Lagerfeld, Alexander McQueen, Gianni Versace, Alexander Wang, Giorgio Armani, Marc Jacobs (Louis Vuitton) Domenico Dolce na Stefano Gabbana, Tom Ford na wengine. Na hata kwa Tanzania wapo wengi wanaofahamika wazi.
Karl Lagerfeld
Japokuwa mambo yanabadilika na hasa kwa nchi za wenzetu na kukubalika kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, kumefanya mashoga nao wafanikiwe kwenye fani zinazotawaliwa na wanaume wa kawaida, lakini mifano ya dunia halisi inabaki michache na hasa tu kwenye majiji ama nchi ambazo mashoga na wasagaji wanapewa heshima sawa na wengine.
Pia kihistoria mashoga kwenye fashion walikuwa wakipewa kipaumbele zaidi kuliko wanawake. Ni Coco Chanel pekee ndio alikuwa miongoni mwa wanawake wachache waliofanikiwa kwenye kiwanda hicho kilichokuwa kikitawaliwa zaidi na mashoga Christian Dior na Cristobal Balenciaga.
Dolce & Gabbana
Pili, inasemekana kuwa utamaduni wa ushoga huwapa nafasi watu hao uwezo wa ubunifu. Mashujaa kwenye jumuiya ya mashoga sio wachezaji wa soka ama wanajeshi- japo wapo. Lakini zaidi wapo kwenye muziki, uigizaji, utengezaji wa filamu, uandishi na sanaa zingine.
Hii ni kwasababu ya ukweli kwamba hizi ndio zilikuwa kazi ambazo mashoga waliweza kufanikiwa na kuendelea kuwa walivyo na kujivunia wanachokifanya. Uwezo wao wa ubinifu huongezeka na ile sense ya upekee ambayo mashoga huikuza ndani ya ulimwengu wa mapenzi ya jinsia mbili (heterosexual world).
Tom Ford
Pointi ya msingi: Upenzi wa mashoga katika urembo, utanashati hauwezi kuelezeka. Inasemekana kuwa mwanaume anayebuni nguo nzuri kwa mwanamke aidha hutaka kuwa na mwanamke ama hutaka kuwa mwanamke’
Credit: Bongo 5
JK amuweka kitanzini Profesa Kapuya
RAIS Jakaya Kikwete ameviagiza vyombo vya dola kuhakikisha vinamkamata mtu yeyote bila kujali cheo, atakayebainika kumbaka au kumuoa mwanafunzi wa shule.
Ametoa kauli hiyo huku aliyekuwa waziri wa wizara tofauti katika awamu mbalimbali za uongozi, Profesa Juma Kapuya, akiandamwa na tuhuma za kumbaka na kutishia kumuua binti, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16.
Ingawa Rais Kikwete hakutaja jina, lakini ni dhahiri kuwa kauli hiyo inamgusa pia Profesa Kapuya, Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM).
Akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara kwenye wilaya za Itilima, Meatu na Maswa mkoani Simiyu, Rais Kikwete alisema mtu anayefanya mapenzi na wanafunzi lazima akamatwe, ahojiwe na kufunguliwa mashitaka ya ubakaji na si vinginevyo.
“Kuna watu wanafanya mapenzi hadi na wanafunzi wakati sote tunajua ukimwi upo na hauna dawa na unaua. Kwa hiyo kila mmoja wetu awe makini kujikinga nao na tuepuke kuwaambukiza wengine,” alisisitiza Rais Kikwete.
Wakati Rais Kikwete akisisitiza wahalifu wa makosa ya kubaka na kuoa wanafunzi wachukuliwe hatua, polisi jijini Dar es Salaam wamekuwa wakisuasua kumchukulia hatua Profesa Kapuya licha ya binti anayedaiwa kumbaka, kufungua jalada namba OB/RB/21124/13 katika kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam, akidai kutishiwa kuuawa na mbunge huyo.
Kauli ya Rais Kikwete imeonyesha dhahiri kukerwa na moja ya ujumbe mfupi wa maneno wa simu ya mkononi kutoka kwenye simu inayodaiwa kumilikiwa na Profesa Kapuya kwenda kwa binti aliyebakwa, ambapo mbunge huyo alijigamba kwamba serikali haiwezi kumfanya chochote.
Ujumbe huo unasomeka hivi: “Mkiuawa itakuwa vizuri…itawapunguzia gharama za kuishi, usitake kugombana na serikali mtoto mdogo kama wewe, sisi ndiyo wenye nchi yetu, mwenye hilo gazeti ni Mbowe, sasa mwambieni nyumba ya kuishi si mmemuingizia hela leo?
Mnatumika tu bure watu wanaingiza hela nyingi, ila mmenitibua lazima niwaue, wiki hii haitaisha, nitapiga kambi kote, jana si wamekuficha, tuone utalindwa milele, maana washatengeneza hela, lazima mvae sanda tu, hilo sio ombi ni wajibu wenu, mnajitia na nyie mafia watoto siyo, watoto wetu wanauza unga nani anawakamata? Nani atapingana nasi.”
Habari kutoka Ikulu ya Rais Kikwete zinaeleza kuwa kiongozi huyo wa nchi amekerwa na kauli ya mbunge huyo wa Urambo Magharibi kwamba serikali haiwezi kumfanya jambo lolote.
Ni kutokana na kauli hiyo, mtoa taarifa wetu alisema rais aliagiza vyombo vya dola kufuatilia kwa karibu sakata hilo na kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake.
Pamoja na msimamo wa Rais Kikwete na binti anayedaiwa kubakwa kuripoti polisi, Profesa Kapuya alifanikiwa kusafiri nje ya nchi huku polisi wakimshuhudia bila kumtia mbaroni.
Akiwa nje ya nchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alikaririwa mara kadhaa akijigamba kuwa polisi inamsaka mbunge huyo na itamtia mbaroni mahala popote alipo.
Hata hivyo, Profesa Kapuya alirejea nchini juzi huku polisi wakimshuhudia bila kuchufkua hatua zozote.
Mwanafunzi huyo anadai kubakwa na Profesa Kapuya kwenye moja ya hoteli ya kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho ndani ya ofisi yake katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipomuita kwenda kuchukua ada.
Source: Tanzania Daima
Source: Tanzania Daima
Ni Tshs. 20,000/= tu Kushuhudia Fainali za Bongo Star Search (BSS) hapo Kesho J'mosi Nov 30, 2013
Najua Watanzania wameshuhudia foleni kubwa sana ya Bongo star search 2013 kupitia TV, Magazeti na hata kusikia kwenye Radio kuhusu waliojitokeza kushiriki ila mshindi ni mmoja na atajulikana Jumamosi November 30 2013 kwenye fainali ambazo nimeambiwa zinafanyika ufukweni, sehemu inayovutia na salama kabisa kwa kila mtu.
Nimeambiwa pia Mshindi anajichukulia milioni 50 ambapo waliofanikiwa kuingia fainali ni Amina Chibaba (MBEYA), Melisa John (DSM), Elizabeth Mwakijambile (DSM), Emmanuel Msuya (MWANZA) na Maina Thadei (DSM) ambapo kabla ya mshindi kutangazwa, Snura, Barnaba, Young Killer, Shaa, Walter Chilambo, Peter Msechu na Makomandoo watapewa nafasi ya kumiliki stage.
VIP unaimiliki kwa 50,000/ na huku kwingine ni 20,000/=ambapo tiketi za siku ya Fainali zinapatikana Shear illusion, Biggy Respect (Kariakoo) Steers Mjini, Zizzou Fashion (Victoria na Sinza) Photo Point (Mayfair) Robby One Fashion (Kinondoni) Best Bite, Engen Mbezi, Escape One (Mikocheni), Benchmark Office Mikocheni, American Nails (Kinondoni).
HATARI:Kasi ya Maambukizi ya Ukimwi yaongezeka Zanzibar..!
RAIS wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein anatazamiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yatakayofanyika Paje Mkoa wa Kusini Unguja .
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kamishina ya Ukimwi Zanzibar (ZAC) Dk Omar Shauri Makame .
Katika mkutano wake na waandishi wa habari alisema kwamba maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika wakati kunaonekana kuwapo na ongezeko la maambukizi mapya.
Alisema katika mwaka 2012-2013 watu 108 walikutwa na maambukizi mapya na kufanya idadi ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi kufikia 6,125 kwa mujibu wa takwimu za watu waliofika katika vituo vya afya kuchunguza afya zao ikiwemo damu.
“Utafiti wa takwimu za ugonjwa wa Ukimwi zinaonesha kwamba yapo maambukizi mapya ya ugonjwa huo kwa kiwango kikubwa ambapo juhudi za makusudi zinahitajika,”alisema.
Kwa mfano alisema Tume ya Ukimwi imeweka mikakati kuyadhibiti makundi hatarishi ikiwemo vijana wanaotumia dawa za kulevya ambapo maambukizi ya kundi hilo yapo kwa asilimia 25.
Mapema Dk Shauri aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi wiki ijayo ambapo ujumbe ni mapambano ya Ukimwi kwa wote yakiwa na lengo la kuwashirikisha watu wenye rika tofauti.
Maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kwa Zanzibar yapo kwa asilimia 14 kwa zaidi ya miaka mitano sasa.
JOSE CHAMELEONE KUWARUSHA WAKAZI WA MWANZA DECEMBER 24 KWENYE MKESHA WA CHRISTMAS
Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisaini mkataba wa wa kupiga show jijini Mwanza itakayofanyika tarehe 24/12/2013 katika mkesha wa kuikaribisha sikukuu ya Christmas kuanzia saa 12 jioni hadi majogoo, tukio linalotazamiwa kufanyika katika ufukwe wa Charcoal Ribs Mwanza
----------------
Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone anatarajia kuwaburudisha wakazi wa jiji la Mwanza kwenye mkesha wa Christmas, December 24.
Ben ambaye ni moja kati ya mapromota waliomsainisha Chameleone mkataba wa kupiga show hiyo amewahakikishia wakazi wa jiji hilo kuwa show hiyo itakayofanyika eneo la ufukweni (Charcoal Ribs) itakuwa ya ubora wa hali ya juu.
"Tutafunga sound mpya ya mtikisiko, tutajenga jukwaa kubwa bora tena la kisasa, tutafunga taa za kisasa pamoja na huduma nzuri kwa wateja watakaofika ufukwe wa Charcoal Ribs Mwanza, nia na madhumuni kuufanya usiku huo kuwa mkubwa, mzuri wenye mengi maajabu katika burudani" Amesema Ben.
PRODUCER ALIYEFUKUZWA KAZI NA WEMA SEPETU KWA KUFANYA MAPENZI KWENYE GARI YA KAMPUNI ANENA MAZITO NA MADUDU YA KAMPUNI HIYO
Baada ya juzi kati kuripotiwa habari ya aliyekuwa producer ama mtengenezaji wa vipindi vya Wema Sepetu Chidi Mohamed kufukuzwa kazi kutokana na kulitumia gari la kampuni kama sehemu yake ya kuvunjia amri ya sita na wadada wa mjini, hatimaye katika pitapita zetu za mtandaoni tuliweza kukutana na kauli ya producer huyo akizungumzia habari hiyo ya yeye kufukuzwa kazi kwenye kampuni ya Endless Fame ya wema sepetu.
Chidi mwenyewe anasema kuwa habari hizo si za kwel na ni kwamba wote walioandika wamepanga kumchafua tuu kwa kuogopa kuwa anaweza kuyaniika mambo mazito yanayoendelea huko endless Fame
Kwa mujibu wa chidi anasema kuwa yeye ameondoka kwenye Kampuni hiyo siyo kwa sababu ya uzinzi ngani ya gari kama ilivyoripotiwa bali ni kutokana na sababu hizi kuu mbili.
1. Ameona hamna jipya na wala hamna maendeleo yoyote ndani ya Kampuni hiyo ndio maana ameamua kuondoka
2. Wafanyakazi wa Endless Fame hawalipwi kabisa ndio maana yeye akaamua kujitoa kwani anafanya kazi bure na pia sio yeye peke yake aliyeondoka bali kuna wafanyakazi zaidi ya watatu walioondoka kwenye kampuni hiyo ila nashangaa ni kwanini wameamua kumchafua yeye?
Bado tunafanya mawasiliano na Endless Fame ili tujue kama daia haya ni ya kweli au la..Endelea kuwa na kilelechahabari BLOG.
MCHAWI ADONDOKA WAKATI AKIENDA KUWANGA
MWANAUME anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 70 ambaye anasadikiwa kuwa ni mchawi, juzi Jumatano alikutwa pembeni ya Mto Okrudu eneo la Kaimebre, sehemu ambayo ni karibu na soko jipya la Kasoa kwenye jiji hilo lililopo katikati mwa nchi ya Ghana.
Jamaa huyo, ambaye alisema kuwa anaitwa Charles Atta, alionekana akiwa hoi huku matiti yakionekana kama ya msichana mdogo.
Mwili wake ulikuwa umetapaka michanga na matope kutoka kwenye mto huo pembeni na alipokutwa, inaaminika jamaa huyo alianguka toka kwenye ungo akiwa kwenye safari zake.
Ndugu wawili ambao ni mtu na kaka yake Liberty Obeng na Innocent Obeng, walisema kuwa walisikia sauti ya ya mtu wasiyemfhamu akilia kutaka msaada.
Kwa mujibu wake, anasema yeye na wenzake walikuwa wanapaa kwenye usawa wa Kanisa ambao unalindwa na Malaika usiku kucha na ndipo alipojikuta ameanguka kwenye eneo hilo la Shule ya Kimataifa ya Watumishi wa Wafalme.
BINTI WA MIAKA 16 ANASWA LAIVU AKIJIUZA AKIWA NA MTOTO WAKE MGONGONI.
Ama kweli shida haina aibu wala huruma! Binti wa miaka 16 aliyetajwa kwa jina la Mama K, amenaswa laivu akifanya shughuli haramu za uchangudoa akiwa na mwanaye mgongoni, akidai chanzo cha kufanya hivyo ni kutokana na shida inayoiandama familia yake.
Binti huyo alibambwa hivi karibuni akijiuza huku mgongoni akiwa na mwanaye wa mwaka mmoja katika Barabara ya Uhuru (kwenye taa za kuongozea magari), jijini hapa.Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ambayo imetinga rasmi mkoani hapa ilinasa tukio hilo usiku wa manane ambapo ilifanikiwa kufanya mahojiano na Mama K aliyekuwa na wenzake wengi walio chini ya miaka 18.
OFM ilichukua maelezo pamoja na picha za mnato huku wenzake wakitoka nduki baada ya kuona mwanga wa kamera.
Cha kushangaza, wakati akihojiwa na OFM, Mama K alidai kuwa haogopi kupigwa picha kwa sababu alishanaswa na kuhojiwa runingani kuhusiana na ishu ya kujiuza hivyo siyo ishu kwake na wala haoni aibu.
Huku akiwa na mwanaye mgongoni, binti huyo alidai kuwa amekuwa akijiuza kutokana na ugumu wa maisha.
OFM: Wewe unatokea maeneo gani na ulianza lini kujiuza?
Mama K: Mimi ni mwenyeji wa Misungwi (wilaya), kwa hapa mjini naishi Mabatini. Sikumbuki nilianza lini lakini yote hii ni kutokana na ugumu wa maisha.
OFM: Huyo mtoto mgongoni ni wa kwako?
Mama K: Ndiyo ni mwanangu wa kumzaa, ana zaidi ya mwaka. Nilijifungua nikiwa na umri wa miaka 15.
OFM: Baba wa mtoto yuko wapi?
Mama K: Sijui.
OFM: Ukipata mteja unamuweka wapi mtoto au unaenda kulala naye na mwanaume?
Mama K: (huku akiondoka) Nawaachia wenzangu.
Katika kujikusanyia data za kutosha, uchunguzi wa OFM uliogusa viunga mbalimbali jijini hapa ulibaini kuwa biashara hiyo haramu imeshika kasi ya ajabu ikihusisha vitoto vidogo kati ya umri wa miaka 12 hadi 16.
Kuhusu bei, tofauti na Dar ambako bei huwa ni ghali, jijini hapa vibinti hivyo vidogo hujiuza kwa kati ya shilingi elfu saba hadi kumi na tano kwa usiku mzima. Hakuna mambo ya ‘short time’.
Katika kubainisha ukweli wa mambo kuhusiana na vitendo vya ukahaba ndani ya Jiji la Mwanza, OFM ilimtafuta meya wa jiji hilo ambapo simu yake ya mkononi haikupatikana hewani.
Akizungumzia na gazeti hili kuhusiana na ishu hiyo ya watoto wadogo kujihusisha na biashara hiyo haramu ya ngono, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo alikuwa na haya ya kusema:
“Sina taarifa yoyote kuhusiana na watoto hao wanaojiuza ndiyo nasikia kwako labda unipe muda niongee na uongozi wa chini nitalichukulia hatua mara moja.”
-GPL
BEIBY MADAHA AMNYONYA DENDA MKE WA MTU MBELE YA MUMEWE..!
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni kwenye Bar ya Uhuru Peack iliyopo maeneo ya Vijana ambapo Beiby Madaha ambae alikuwa tungi kipita kiasi alianza kumlazimisha dada huyo kumla mate baada ya kumsifia kwa kazi nzuri anazozifanya msanii huyo.
Mariam Mndeme na Beiby Mdaha |
AIBU:WANAWAKE MTAKUWA WATUMWA WA MAPENZI MPAKA LINI..?? TAZAMA HUYU DADA ALIYEKUBALI KUCHEZA *UCHI* ILI ASIACHWE NA MPENZI WAKE
Ulimbukeni wa mapenzi umeendelea kuwaangamiza akina dada wenye kupenda miteremko....
Wengi kati yao wamejikuta wakiishia kuwa watumwa wa penzi kwa kukubali ama kupigwa picha za uchi au kurekodiwa video wakiwa uchi eti kwa kisingizio kwamba kukubali kupigwa uchi ni udhihirisho kwamba anampenda boy wake na kwamba hatamsaliti....
Huyu dada ni miongoni mwa watu waliodanganyika na imani hiyo .Amekubali kurekodiwa akicheza uchi huku mpenzi wake akimpapasa makalio yake...
Kinachotia huruma ni kwamba, baada ya mpenzi wake kumaliza haja zake, Video ilisambaa na hatimaye nasi tukainasa ikiwa mitandaoni...
Bofya hapo chini uingie jukwaa la wakubwa ujionee
oNYOkali..
Ukipiga picha ya utupu kwa namna yoyote ile..Jua iko siku utaacha hadharani..wakina dada kuweni makini..Hii sio vizuri
Friday, November 29, 2013
"Kama kuna wanawake wanataka kuzaa na mimi muda wowote nawakaribisha...."....Baba Kanumba
BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa amefunguka kuwa baada ya kutangaza kuwa wanawake wanaotaka uzao wake wajitokeze azae nao, wamejitokeza kumi lakini akawapa masharti, yakawashinda.
Akizungumza na mwandishi wetu, baba Kanumba aliweka bayana kuwa warembo hao waliojitokeza aliwapa sharti la kwenda kupima Ukimwi lakini ajabu wote waliingia mitini.
“Wamejitokeza vizuri lakini nashangaa wote wamekuwa wazito katika suala la kupima Ukimwi wameingia mitini, kama wapo wengine watakaolimudu sharti hilo, nawakaribisha,” alisema baba Kanumba
Akizungumza na mwandishi wetu, baba Kanumba aliweka bayana kuwa warembo hao waliojitokeza aliwapa sharti la kwenda kupima Ukimwi lakini ajabu wote waliingia mitini.
“Wamejitokeza vizuri lakini nashangaa wote wamekuwa wazito katika suala la kupima Ukimwi wameingia mitini, kama wapo wengine watakaolimudu sharti hilo, nawakaribisha,” alisema baba Kanumba
Baba wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa. |
Kada wa CCM Zanzibar Acharangwa Mapanga kama Mdudu wakati akitoka harusini Nyakati za Usiku..!!
Kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM Jimbo la Mpendae, Hassan Abdallah Said (25) ameshambuliwa kwa mapanga wakati akitoka harusini saa tano usiku.
Akizungumza na Mwananchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Khamis Mkadam alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema maafisa wa upelelezi wameanza kufanya uchunguzi.
Makadam alisema uchunguzi wa awali umemwonyesha kuwa kijana huyo alishambuliwa na watu wasiojulikana kabla ya kupelekwa Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa matibabu .
“Ni kweli tukio hilo limetokea, tumeanza kufanya uchunguzi ikiwemo kutafuta taarifa muhimu zitakazosaidia uchunguzi wetu kufanikiwa kuanzia katika eneo la tukio na kuhakikisha waliofanya uhalifu huo wanakamatwa,” alisema Mkadam
“Ni kweli tukio hilo limetokea, tumeanza kufanya uchunguzi ikiwemo kutafuta taarifa muhimu zitakazosaidia uchunguzi wetu kufanikiwa kuanzia katika eneo la tukio na kuhakikisha waliofanya uhalifu huo wanakamatwa,” alisema Mkadam
Hata hivyo Mkadam alisema ni mapema kuzungumzia chanzo cha tukio hilo na kuwataka raia wema kuwasaidia kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu.Akizungumza kwa shida huku akiwa hospitali, majeruhi Hassan alisema alikuwa akitoka kwenye sherehe ya harusi na kuitwa na watu wawili akitakiwa asimame.
“Niliitwa na kufikiri kama ni utani, waliniita wee CCM mjinga hebu simama, nikasimama na ghafla wakaongezeka wengine na kuanza kunishambulia kwa mapanga,” anaeleza Hassan. Hassan alieleza kuwa shambulio hilo ni la kisiasa na kwamba anawafahamu vijana wawili waliokuwa wakishiriki harakati za Jumuiya ya Uamsho.
Subscribe to:
Posts (Atom)