aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, October 3, 2013

WATOTO WENGINE WAKAMATWA WAKITAKA KUPANDA NDEGE KWENDA NJE YA NIGERIA.....


Mtoto mmoja alikamatwa kwenye uwanja wa ndege huko Nigeria baada ya kujificha kwenye vyumba vya matairi ya ndege na kusafiri kutoka Benin hadi Nigeria, mtoto mwenyewe alidhani ndege inakwenda Marekani ambapo baadae huyu mtoto alipewa scholarship kwenye moja kati ya shule nzuri hukohuko kwao Nigeria.
Baada ya muda mfupi wamekatwa watoto wengine lakini hawa walikuwa bado hawajapanda ndege ambapo taarifa kutoka Nigeria zinasema watoto watatu wawili wana miaka 14 na mmoja 13, wamekatwa Murtala Mohammed International Airport wakiwa wanajaribu kupanda ndege yoyote ili wasafiri kwenda nje ya Nigeria.
Wawili walikamatwa kwenye eneo ambalo abiria wanaosafiri wanapita (Departure) kuelekea kupanda ndege zao ambapo Askari walipoanza kuwauliza kuhusu documents za kusafiria lakini wote walikosa cha kujibu na baadae mmoja wao alijitetea kwamba kaja kushangaa ndege.
Baadhi ya vyombo vya habari na watu mbalimbali nchini Nigeria kwa pamoja wametoa lawama juu ya scholarship aliyopewa mtoto wa kwanza kuwa imekuwa chachu kwa watoto wengine kufanya kama alivyofanya yeye.
Siku ambayo mtoto wa kwanza Daniel Ikehina alivyokamatwa airport Nigeria
 
Hapa ni siku akikabidhiwa scholarship

No comments:

Post a Comment