aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, October 4, 2013

BIBI TITI ALIVYOPANGA KUMUUA NYERERE

Bibi Titi na Mwalimu wakihutubia wananchi enzi za TANU.
WIKI iliyopita niliandika juu ya kesi ya uhaini iliyoanza kunguruma Juni 8, 1970 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar.
Niliwataja pia baadhi ya watuhumiwa waliofikishwa mahakamani lakini mtuhumiwa mmoja alishangaza wengi na si mwingine isipokuwa ni Bibi Titi Mohammed (45).
Wengi walishangaa na kujiuliza, mama huyu kweli alitaka kumuua Rais Julius Nyerere? Walijiuliza hivyo kwa sababu enzi hizo mwanamke kujihusisha na kitu kizito kama hicho ilikuwa ni ndoto, lakini yeye alifanya na alimwaga fedha kwa kazi hiyo.
Lakini pia wananchi walishangaa kwa kuwa Bibi Titi aliwahi kuwa waziri na rais wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT).
Kama ilivyo kwa watuhumiwa wengine ambao walikuwa na majina bandia ya ‘kazi’. Mama huyo naye mahakama iliambiwa alikuwa na majina mengine aliyojiita au kuitwa nayo ambayo ni Mama Mkuu, Mwamba au Anti wakati wa mipango yao ya mauaji na kuipindua serikali ya Nyerere.
Bibi Titi aliyezaliwa mwaka 1926 alikuwa kivutio kila alipokuwa anafikishwa mahakamani kwani wakati wa ujana wake alikuwa mtu wa karibu wa Nyerere.
Alishirikiana wakati wa kudai uhuru na hata baada ya taifa kuwa huru. Ilielezwa kuwa Bibi Titi aliunganishwa kwa Nyerere na dereva mmoja wa teksi ya nyumbani kwao mwaka 1954  na akawa mmoja wa waanzilishi wa chama cha Tanu.
Biti Titi alikamatwa na polisi Oktoba 1969 akiwa na waziri wa zamani wa kazi, Michael Kamaliza pamoja na maofisa wanne wa JWTZ na wote wakafunguliwa mashitaka ya kutaka kumuua na kumpindua Nyerere.
Ushahidi mwingi ulitolewa mahakamani na ilielezwa kuwa alikuwa akimwaga fedha ili kufanikisha mpango huo haramu kutokana na ufadhili wa mtu mmoja ambaye alikuwa nje ya nchi.
Je, nani alikuwa akimpa fedha? Utapata majibu haya katika toleo lijalo.
SOURCE:GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment