aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Saturday, October 5, 2013

AJALI MBAYA YA MLIMA KITONGA YAUA WAWILI....


Ajali mbaya  nyingine  imetokea  usiku  huu katika mlim
a kwa Kitonga wilaya ya Kilolo mkoani Iringa katika barabara  kuu ya Dar es Salaam -Iringa . 

Katika  ajali  hiyo  watu  wawili wamekufa papo hapo huku
watu  wawili  wakijeruhiwa  vibaya baada ya malori mawili kugongana uso kwa uso . 


 Ajali  hiyo imetokea  mida ya saa 12.50 jioni ya  leo  ikiwa ni dakika takribani 30  baada ya ajali ya basi la JM kupinduka eneo  la Mazome wilaya ya Kilolo. 

Basi  la  JM lilipinduka  mida  ya  saa  kumi  na  mbili  na dakika  20  na  kujeruhi  watu  15
Chanzo ni dereva  wa lori la IT lililokuwa  likisafirishwa kwenda nchi  za  kusini mwa Tanzania aliyekuwa akitaka  kulipita gari la mbele mlimani na katika kona kali .

Dereva  wa  lori  hilo la  IT aliyetambuliwa kwa jina la Gody amevunjika mguu  wake na dereva  na utingo la fuso wamekufa papo hapo  huku mwanamke  aliyekuwa katika lori la IT akisalimika . 


Credit: Paparazihuru

No comments:

Post a Comment