aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, August 5, 2013

MANCHESTER UNITED YATHIBITISHA KUKATAA OFA MPYA YA CHELSEA KWA WAYNE ROONEY

Manchester United wamethibitisha kwamba wamekataa ofa ya pili 
ya Chelsea kwa ajili ya kumsaini mshambuliaji wao Wayne Rooney.
Jose Mourinho tayari alishaona ofa yake ya kwanza inayokadiriwa 
kuwa £20m kwa jili ya mshambuliaji huyo wa England  ikikataliwa 
lakini pia ofa yake mpya inayokadiriwa kuwa £30m nayo imepigwa 
chini.
Mourinho alikiri mwezi uliopita kwamba Rooney ndio chaguo lake 
pekee la usajili lilobaki, wakati mchezaji husika akiripotiwa kuwa 
tayari kulazamisha kuuzwa kwa kuandika ombi la kuuzwa rasmi.  

Boss United David Moyes ameshasema mara kwa mara kwamba
 mshambuliaji wakemwenye miaka 27 hauzwi na msemaji rasmi 
wa klabu hiyo amezungumza tena leo asubuhi. 

"Jana tulipokea ofa kutoka kwa helsea, na kwa haraka ilikataliwa,
" alisema msemaji huyo wa United. "Msimamo wetu bado haujabadilika
 kwamba Rooney hauzwi."
Rooney, ambaye bado ana miaka miwili iliyobaki kwenye 
mkataba wake, anategemewa kusafiri 
na timu mpaka Sweden leo jioni, kuelekea mchezo 
wa kirafiki dhidi ya AIK jijini Stockholm kesho jumanne.
Moyes ameripotiwa kumuudhi sana Rooney wakati aliporipotiwa akisema 
kwamba Rooney atakuwa back up ya Van Persie ikiwa mshambuliaji huyo 
aliyehamia kutoka Arsenal angepata majeruhi.

Graeme Souness anaamini Manchester United wamejiweka kwenye 
sehemu
 mbaya na namna wanavyoshughulikia suala hilo, lakini kamwe 
hawatomuuza kwa klabu ya England. 

Alisema: "Maneno ya Moyes yamemfanya Rooney akasirike sana. 
Kuambiwa kwamba atakuwa chaguo la pili baada ya Van Persie 
kumeumiza hisia zake.
"Manchester United wamejiweka kwenye nafasi mbaya kwenye 
suala hili, lakini sidhani kama watamuuza kwa klabu ya Premier League."

No comments:

Post a Comment