aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, August 30, 2013

Uchambuzi Yakinifu wa Kitakwimu Sakata la Rwanda na Uganda kujitoa bandari ya Dar es Salaam!

Takwimu zasema kwa sauti kuliko Siasa!

1. 68% ya mizigo ya Rwanda inapita bandari ya Dar ikilinganishwa na 41% miaka 5 iliyopita. 47% ya gharama za usafirishaji wa mizigo ya Rwanda inatokana na gharama za ziada (overhead) za kupitishia bandari ya Mombasa Inakadiriwa, gharama ya kusafirisha kontena kutoka Mombasa hadi Kigali ni $ 5,000, kati ya hizo $ 1,500 ni gharama zitokanazo na urasimu na ucheleweshaji.;

2. 2% tu ya mizigo ya Burundi inapita bandari ya Mombasa hivyo zaidi ya 90% hupita Dar es Salaam;

3. 1% ya mizigo ya Uganda (tani milioni 4) hupita bandari ya Dar es Salaam sasa hivi ikilinganishwa na 5% ya mizigo ya Uganda iliyokuwa ikipita bandari ya Dar mwaka 2004;

4. Umbali kati ya Mombasa- Kigali ni 1700kms, na mzigo unapita kwenye mipaka miwili . Umbali wa Dar-Kigali ni 1300kms na mzigo hupita kwenye mpaka mmoja tu. Tofauti ya umbali kati ya Mombasa- Kigali na Dar-Kigali ni 400kms ambazo ni sawa na umbali wa kutoka Dar-Mtwara. 

5. Kuna vizuizi (road blocks) 36 kati ya Mombasa-Kigali na vizuizi 30 kati ya Dar-Kigali. Inakadiriwa kuchukua siku 20 kupakua na kutoa kontena Mombasa kufikisha Nairobi, siku 22 kulifikisha Kampala na siku 24 kulifikisha Kigali, wakati inachukua siku 7-14 kulitoa Dar kulifikisha Kigali;

6. Uwezo wa Bandari ya Mombasa ni kuhudumia wastani wa konteza za futi ishirini 600,000 teu kwa mwaka. Uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam ni kuhudumia wastani wa 500,000 teu kwa mwaka. Kwa sasa Mombasa inahudumia wastani wa 903,000 tu kwa mwaka na Dar wastani wa 580,000 tu kwa mwaka.

Ukipitia takwimu hizi, kinachojitokeza wazi ni kuwa, suala la kutumia au kutotumia bandari ya Dar es Salaam haliwezi kuwa suala la uamuzi wa kisiasa bali kibiashara. Sehemu kubwa ya wasafirishaji wa mizigo hii sio Serikali bali wafanyabiashara/sekta binafsi. Tanzania imepewa upendeleo wa kijiografia, kinachotakiwa ni jitihada kidogo kuboresha mifumo na kuongeza ufanisi katika bandari na sekta ya barabara. Uamuzi wa matumizi ya bandari ni uamuzi wa kiuchumi/ kibiashara si kisiasa.

No comments:

Post a Comment