aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 28, 2013

KIFAA CHA TMA KILICHOZUA TAHARUKI KWA WAUMINI WA KKKT KIJITONYAMA

Kifaa cha TMA kilichozua sintofahamu kwa waumini hiki hapa.
Kifaa hicho kikionyeshwa kwa wananchi, waumini na wanahabari.
 Kifaa cha TMA kikitolewa katika transfoma.
Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi na waumini wakiwa katika taharuki baada ya kuonekana kifaa hicho.

Watu wa dharura wakiondoka baada ya kubaini kuwa ni kifaa cha TMA.

JUZI (Jumapili) hali ya taharuki ilizuka kwa waumini wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam baada ya kuonekana kifaa cha Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kilichosadikiwa kuwa bomu.
Kifaa hicho ambacho kilifungwa katika boksi kilikutwa juu ya transfoma umbali wa takribani meta 20 kutoka nje ya kanisa hilo.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jana, Mtabiri Mwandamizi wa TMA, Agustine Kanemba alisema kifaa hicho huwa kinarushwa kila siku kwenda angani kwa urefu wa kilometa 55,000 kikiwa kimeambatana na puto.
Alisema kikifika huko puto hupasuka na kusababisha kifaa hicho kudondoka chini jambo ambalo linasababisha wao kupata taarifa za hali ya hewa ya anga baada ya hatua hiyo.

No comments:

Post a Comment