Tetesi za kiungo mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs
kuwa mbioni kujiunga na klabu
kuwa mbioni kujiunga na klabu
ya Real Madrid zimezidi kushika kasi baada ya klabu hiyo kushusha picha ya kiungo huyo
kwenye ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa twitter.
Ukurasa wa Twitter wa klabu ya Tottenham ulikuwa na picha kubwa za wachezaji Gareth
Bale na Clinton Dempsey lakini picha hizo zilitolewa baada ya Dempsey kujiunga na
timu ya Seattle Sounders ya Marekani.
Kuondolewa kwa picha ya Bale ndio kumezua gumzo kubwa kwani inaonyesha
kuwa tayari Spurs wameanza kuchukua hatua za kusonga mbele na kuanza maisha
bila ya nyota huyo ambaye kwa kiasi kikubwa ametokea kuwa alama ya klabu hiyo.
Wiki iliyopita nyota huyo wa kimataifa wa Wales aliwaaga wachezaji wenzie kwenye
kikosi cha Spurs Saa chache kabla ya wachezaji hao kuondoka kwenda nchini
Ufaransa ambako walikuwa wanacheza mechi ya Kirafiki dhidi ya Monaco .
Real Madrid na Tottenham zimekuwa kwenye mazungumzo juu ya usajili wa
Bale na mazungumzo hayo yamechukua muda mrefu kutokana na msimamo wa
klabu hiyo ya London wa kutaka fedha yote huku Madrid wakitaka kulipa kwa
awamu .
Pamoja na mazungumzo hayo kuchukua muda mrefu Madrid wanatarajia
kumthibitisha Bale kama mchezaji wao siku yoyote kabla ya kumalizika kwa kipindi
cha usajili wakati wa majira ya joto.
No comments:
Post a Comment