aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 7, 2013

Huyu ndio msanii aliesababisha promota kupigwa faini ya milioni zaidi ya 15




El Komander 2
Mamlaka za Chihuahua Mexico zimempiga faini
 ya zaidi ya milioni 15 za Kitanzania promota wa
 matamasha ya muziki kutokana na kukiuka sheria 
ambayo inazuia upigaji wa nyimbo zinazotukuza au
 kusifia matumizi ya dawa za kulevya.
Hii imetokana na tamasha lililofanyika July 27 2013
 ambapo msanii El Komander alifanya show na kuimba
 nyimbo zake zenye mistari inayotukuza matumizi ya
 dawa za kulevya na tamaduni nyingine za kihuni.
El Komander ambae ana video zilizotazamwa na 
mamilioni kwenye youtube zinazoonyesha akiwa 
na bunduki, magari ya spidi kubwa na dawa za kulevya 
aina ya cocaine zikiwa zimetazamwa na mamilioni ya 
watu, amekanusha kuhusika na tamasha hilo.
El KomanderKomander amewaambiwa waandishi wa habari 
kwamba yeye anapata nafasi ya kwenda kila mahali
 kwa sababu ni raia mwema na anafata sheria ya kila
 area, huku akisisitiza “sisi tukiambiwa tusiimbe kitu 
flani hatuimbi, tuna nyimbo nyingi ambazo tunaimba
 na tunazifurahia, kama kuna mtu ambae hatupendi, 
hatuwezi kufanya kitu’
Rapper huyo alimwambia promota wa Tamasha 
kuhusu nyimbo zake zote kabla ya tamasha na 
hakufahamu kama kulikua na tatizo lolote ambapo 
sasa msaidizi wa gavana wa jimbo laChihuahua
 amesema hiyo faini ya zaidi ya milioni 15 za
 Kitanzania aliyopigwa promota, itatumika kununua 
computer na vitu vingine kwenye vituo vya jamii.
El-Komander-4-M
Mayor wa Shiwawa Marco Quezada Martínez 
amewaambia waandishi wa habari huo ndio mwisho
 wa promota huyo kupewa kibali cha kuandaa 
matamasha zaid huku akiwasisitiza viongozi wa
 miji mingine kupiga vita nyimbo zinazosifia maovu 
ambayo yameua maelfu ya watu kwenye miaka ya 
karibuni Mexico.
Sheria zinazopinga nyimbo zinazohamasisha matumizi 
ya dawa za kulevya na uovu zimekua zikitekelezwa kama 
hivi kwa muda wa miaka mitatu nchini Mexico, hapo jamaa kashupaliwa tu kinomanoma kisa nyimbo za kusifia dawa za kulevya wala sio kwamba alishikwa na dawa za kulevya wala kuzipitisha Airport.

No comments:

Post a Comment