Watanzania wametakiwa kuitumia vema huduma mpya ya utoaji taarifa za
wahamiaji haramu pamoja na taarifa za waathirika wa biashara hiyo, ili kupata
msaada na kupunguza kasi ya biashara hiyo nchini.
Huduma hiyo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam na shirika la kimatiafa la
Wahamiaji (IOM) kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani, ambapo
Mkurugenzi
wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Haji Janabi ametoa wito wa matumizi sahihi ya
huduma hiyo katika kutoa taarifa za wahamiaji haramu pamoja na vitendo vya biashara
haramu ya binadamu.
Huduma hiyo ambayo ni kitabu chenye namba za simu za vyombo mbalimbali, vikiwemo
vyombo vya dola vinavyotoa msaada wa haraka, imekuja wakati ambapo Tanzania
imekuwa ikishuhudia ongezeko la matukio ya wahamiaji pamoja na biashara
haramu ya binadamu.
No comments:
Post a Comment