Pichani ni Mwili wa Mtu aliyekutwa katupwa katika Msitu wa Kibamba Hospitali na Makondeko Luguruni, ukiwa katika hali mbaya kutokana na kudhaniwa kuwepo kwa takribani siku 4 na zaidi, mpaka sasa hajatambulika kwa jina, kutokana na kuharibika. Kikosi cha Askari kwa kushirikiana na Mjumbe wa Nyumba kumi kumi, Serikali ya Mitaa, kwa pamoja wamekubaliana kuuzika Mwili huo Pale alipokutwa katelekezwa. Hali hiyo imesababisha hofu kwa wakazi wa Maeneo ya Kibamba, Mbezi na Vitogoji vya Jirani. hivyo wameitaka serikali kuongeza jitihada za Ulinzi ususani wakati wa Usiku katika Bonde la Makondeko kuelekea Kibamba Hospitali.
Baadhi ya wakazi wa Maeneo ya Kibamba na Makondeko, wakijaribu kutambua Mwili huo ambao umekutwa Eneo alikokutwa katelekezwa, Bondeni kutoka katika Daraja la Kibamba Hospitali na Makondeko.
Baadhi ya Askari wakiwa eneo la Tukio kwa Maziko na Uchunguzi.
Baadhi ya wakazi wa Maeneo ya Kibamba na Makondeko, wakijaribu kutambua Mwili huo ambao umekutwa Eneo alikokutwa katelekezwa, Bondeni kutoka katika Daraja la Kibamba Hospitali na Makondeko.
No comments:
Post a Comment