WANAFUNZI wawili wa shule ya msingi Itobo wilaya ya Nzega mkoani wa Tabora wamekufa maji katika bwawa wakati wakiwinda bata mzinga. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Peter Ouma alisema Massanja Shija (42) ambaye ni baba wa mmoja wa watoto hao waliokufa, amenusurika katika tukio hilo baada ya kunasa kwenye tope.
Kamanda alitaja watoto waliokufa ni Elias Massanja (13) na Shabani Ramadhan (15) wote wanafunzi wa darasa la sita shule ya Msingi Itobo. Tukio hilo ni la Julai 30 mwaka huu, saa 12:30 jioni katika Kijiji cha Chamwabo, Kata Itobo.
Ouma alisema walikuwa wakiwinda bata mzinga ambaye aliruka na kwenda kwenye bwawa na katika kumfuata, walizama katika kina kirefu cha maji.
Alisema baada ya kuzama, jitihada za kuokoa miili yao ilikuwa ngumu kutokana na kukosa waokoaji. Hata hivyo baadaye iliopolewa.
Mbunge wa Jimbo la Bukene, Selemani Zedi alisema tukio hilo ni la kusikitisha kwa jamii. Aliwataka wananchi kuwa makini na mabwawa
No comments:
Post a Comment