KIJANA mmoja ambaye hajafahamika jina lake anayedaiwa kuwa ni jambazi amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali eneo la Mbezi kwa Msuguli jijini Dar es Salaam.
Kijana huyo pamoja na mwenzake wakitumia pikipiki walikuwa na silaha za moto tayari kwa kwenda kufanya uhalifu lakini kabla mpango wao haujakamilika polisi waliingilia kati na kuanza kupambana nao.
Haikuwa kazi rahisi kuweza kumkamata jambazi huyo kutokana na majibizano ya risasi kati yake na polisi.
Baada ya jambazi lililokuwa linaendesha pikipiki kuona mwenzake anaelekea kukamatwa lilitokomea wakati mwenzake akiangukia mikononi mwa wananchi wenye hasira kali waliomshushia kipondo cha nguvu.
TAZAMA VIDEO HAPO CHINI....
No comments:
Post a Comment