Real Madrid wapo tayari kumuuza Cristiano Ronaldo
kwenda Manchester Unitedmwezi huu baada ya nahodha
huyo wa Ureno kukataa kuanza mazungumzo ya mkataba
mpya.
Gazeti la Daily Star limesema United na Real Madrid
wametumia siku 12 zilizopita kuzungumza juu ya ada
ya uhamisho ya paundi millioni 80 - na mabingwa wa
Premier League wamezidi kupata uhakika wa kumrudisha
kipenzi chao Old Trafford.
Raisi wa Real Florentino Perez mwanzoni alitaka kwamba
uhakika kutoka kwa Ronaldo kama yupo tayari kusaini
mkataba mpya - na alishangazwa kwamba mchezaji kuwa
alikuwa tayari kurudi United.
Hilo lilipelekea Madrid kufungua mazungumzo rasmi
na United, wakitambua kwamba wanaweza wakamuuza
kwa fedha kidogo ikiwa winga huyo atabakia kwamwaka
mmoja zaidi ndani ya Bernabeu kwa kuwa atakuwa
amebakisha mkataba wa mwaka mmoja tu.
Lakini pia imeonekana wazi kwamba Madrid wanataka
kumpata mbadala wa Ronaldo - Gareth Bale ambaye
tayari wameshatoa ofa ya £85m kwa Spurs.
Mapema wiki hii aliyekuwa raisi wa Madrid - Ramon
Calderon alikaririwa akisema kwamba Madrid
wanajiandaa kumuuza Ronaldo na ndio maana
wanafanya kila liwezekanalo kumsajili Gareth
Bale kutoka Tottenham.
Ikumbukwe pia wakati akiwa bado kocha wa Man
United Sir Alex Ferguson alikarriwa akisema kila
kipo sawa kwa ajili ya usajili wa mchezaji mkubwa
wakati wa dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa.
Pia Wakati akihojiwa na BBC hivi karibuni aliyekuwa
msaidizi wa Ferguson - Mike Phelan aliulizwa kama boss
wake alikuwa akimzungumzia Ronaldo aliposema kuhusu
usajili wa mchezaji mkubwa? Phelan alishindwa kukataa wala
kukubali kuhusu suala hilo, akisema "no comment'.

No comments:
Post a Comment