Kanye West na Kim Kardashian
Rais Obama hajali ushawishi walionao celebrities kwa vijana wa leo. Katika mahojiano ya hivi karibuni na Amazon.com,Obama alisema ushawishi mbaya kama vile wa Kim Kardashian na Kanye West haukuweza kumvuruga kiasi cha kutotekeleza azima yake ya ndoto ya Marekani aliyokuwa nayo tangu utotoni.
Alaumu ushawishi huo mbaya walio nao na show za maisha halisi.
Rais Obama
‘American Dream’ ilihusisha vitu vya msingi ni pamoja na kazi nzuri ambapo watasikia hali ya usalama. Elimu bora ... Watu walidhani kama wakifanya kazi kwa bidii watafika huko.... sidhani kama watu huwa wanajiambia, 'Nahitaji kuwa na nyumba ya miraba 10,000'.... Nadhani, pia kumekuwa na mabadiliko katika utamaduni. Sisi hatukuwekewa mambo wazi kama watoto wa siku hizi. Hakukuwa na dirisha katika maisha ya matajiri na maarufu. Watoto walikuwa hawafuatilii kila siku nini Kim Kardashian alikuwa amevaa au Kanye West anaenda wapi likizo na kufikiri kwamba kwa namna fulani hiyo ilikuwa ni alama ya mafanikio. 'Alisema rais Obama.
No comments:
Post a Comment