MTOTO wa kike ameuawa kinyama kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kisha kunyofolewa macho na ubongo wake.
Tukio hilo la kikatili limetokea mwishoni mwa wiki eneo la Idiwili, Kata ya Isuto, Wilaya ya Mbeya Vijijini, mkoani hapa.
Mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Lilian Kasonso (2) alikatishwa uhai wake kwa makusudi kisha mwili wake kutelekezwa chini ya mti.
Baadhi ya wananchi wa eneo hilo waliozungumza na Tanzania Daima Jumatano, walisema kuwa mama wa mtoto huyo, alimwacha mwanae akiwa salama mikononi mwa bibi yake kisha yeye kwenda kutafuta kuni.
Walisema kuwa baada ya muda bibi yake naye alienda kuchota maji mtoni huku akimwacha mjukuu wake ndipo wakatili hao walitumia mwanya huo na kumteka mtoto huyo kisha kutokomea naye pasipo mtu kuwaona ama kuwashitukia.
“Mama wa marehemu aliporejea na kuuliza mwanae yupo wapi, ndipo ikawa kama amewazindua ndugu waliokuwepo jirani kisha ikapigwa mbiu ya kutaka msaada, wananchi wakasambaa na kuanza kumsaka mtoto Lilian,” walisema.
Walisema wakati wakiendelea na utafutaji walimuona mtu mmoja kwa mbali akiwa amevalia shati jeupe ndani ya mashamba ya kahawa, na walipojaribu kumfuatilia aliwatoroka lakini waliona mwili wa mtoto huyo ukiwa umefunikwa na majani ya kahawa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa atahakikisha anapambana na wakatili hao.

No comments:
Post a Comment