Uwanja wa Ndege wa Nairobi walipuka moto! Hali ya taharuki yatawala
Moto mkubwa wazuka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyetta (JKIA) jijini Nairobi.
Chanzo cha moto huo bado hakijatambulika na juhudi za kuuzima zinaendelea, ambapo vikosi mbalimbali vya zimamoto vipo uwanjani hapo kuthibiti janga hilo.
Habari zinasema hakuna mtu aliyedhurika hadi sasa katika moto huo ingawa hasara iliyopatikana inasemekana ni kubwa na kwamba abiria wengi wamekwama uwanjani hapo. Barabara kuu ya kuelekea JKIA imefungwa.
No comments:
Post a Comment