Huyu msanii mauti yalimkuta katikati ya Uwanja akifanya Vitu vyake katika Uwanja wa shule ya msingi Radienya iliyopo huko Rorya Mkoa wa Mara.
Kwa kweli ni kifo cha kuhuzunisha sana na cha ghafla,na kwa kuwa hali haikuwa nzuri kwa BK Sande ambaye alikuwa bosi wa huyu Densa aitwaye Masta CHEIN,ilibidi azikwe huko huko Rorya kijiji cha Nyarombo.
Kama unavyoona kwa picha ni mazishi ya kuhuzunisha sana.Hata maandalizi
inatia huruma.
BK Sande anadai walitoka Bukoba wakiwa wazima kabisa na kuanza show salama ila kitendo cha dakika 1 akaanguka na kufariki palepale.
Kwao ni Mtwara huyu marehemu hivyo gharama ilikuwa
kubwa kumsafirisha ikabidi azikwe hukohuko.
Mengi amezungumza na babamzazi.com hapo chini.Msikilize.
Mwili wa marehemu ikiwa imelazwa kwenye jamvi kuu kuuu.
Kama unavyoona hata watu walikuwa wachache sana.
Kwa kweli inatia huruma sana.
BK Sande alovaa shati ya Drafti akiwa na madensa wake baada ya kumzika Densa Mwenzao.
Master CHAIN Mtaalamu wa Sarakasi.
Hapa Mwili wa Marehemu ukiwa tayari kuzikwa.Hapa amewekwa juu ya mchanga.Kama unavyoona inatia huruma kwa kweli.Kazikwa bila Jeneza.Hujafa hujaumbika.
Huyu ndio BK Sande aliyefiwa na Densa Wake uwanjani.
No comments:
Post a Comment