aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, August 5, 2013

ELLY G ANUSURIKA KUFA KWA KUNYWA GONGO.....!!

Elia Daniel
                Elly G mwigizaji wa filamu

MWIGIZAJI wa filamu anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu Swahiliwood Elia Daniel ‘Elly G’ hivi karibuni alinisurika kupoteza uhai wake baada ya kunywa pombe ya kienyeji aina ya Gongo, msanii huyo alikutwa na sakata hilo akiwa anarekodi filamu yao ya Kupa maeneo ya Kibaha vijijini Elly G alikuwa yupo katika scene iliyomfanya atumie pombe hiyo. 
.


Elia Daniel
                  Elly G akiwa katika pozi.

Elia Daniel
                   Elly G katika pozi lake matata.
“Nilimuona Israel mtoa roho , siku hiyo nilikuwa nimekunywa dawa aina ya Flagly na dawa nyingine kwa sababu nilikuwa nasumbuliwa na tumbo, hivyo wakati narekodi kuna scene nilitakiwa ninywe pombe ya kienyeji Gongo sasa unajua katika take two take one nikajisahau kama nikunywa dawa nikanywa na kupoteza fahamu,”anasema Elly G.
Msanii huyo ambaye baada ya kunywa pombe hiyo huku akiwa ametumia dawa aliishiwa nguvu na kutokwa na mapovu mdomoni hadi walivyoanza kumpatia huduma ya kwanza na kuokoa maisha yake baada ya kuchanganya na dawa mwenyewe anasema Mungu alikuwa upande wake kwani hata zilizomuokoa ni za asili kwani kutoka sehemu waliyokuwepo hadi kufika Hospitali ni mbali na hakuna usafiri wa haraka
.

No comments:

Post a Comment