Dada wa damu wa mwanasoka ghali zaidi duniani Cristiano
Ronaldo amesaini mkataba mnono wa kutengeneza albam
yake ya kwanza ya muziki na kampuni ya utayarishaji ambayo
hufanya kazi na wasanii wakubwa kama Lady Gaga na J-LO.
Katia Aveiro ambaye single yake ya kwanza "Boom sem parar"
imepata umaarufu mkubwa kwenye mtandao wa Youtube, tayari
ameanza kuunda albam yake na watayarishaji kutoka RedOne huko
jijini Madrid - mahala ambapo ndio ameweka makazi yake ya kikazi.
Ronaldo, ambaye jana alipigwa picha akiwa na mwanamuziki J-LO
amezungumza kuhusu dili hilo la dada yake na kusema:
"Nina furaha sana kwa ajili yake."
Aveiro anatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha kubwa
mwezi ujao jijini Madrid huku albam yake ya kwanza
ikitarajiwa kutoka mwezi November. Alisema: "Huu ni
mwanzo wa muziki wangu kuwa wa kimataifa."
HII NDIO VIDEO YA WIMBO WA KATIA AVEIRO
No comments:
Post a Comment