aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 6, 2013

AJALI MBAYA YATOKEA MBEYA MMOJA AFARIKI PAPO HAPO


GARI AINA YA TOYOTA COROLLA  ILIYOGONGANA NA BASI 
LA HOOD MENEO YA MSWISWI MBEYA DEREVA
 WA GARI NDOGO AMEFARIKI PAPO HAPO
HATI YA KUSAFIRIA YA MAREHEMU DAVIS HANAMUNDE MZAMBIA



MNAMO TAREHE 04.08.2013  MAJIRA YA SAA 06:45HRS HUKO MSWISWI 

WILAYA YA MBARALI BARABARA YA MBEYA/IRINGA, GARI NO T. 159 AXM 
AINA YA SCANIA BUS MALI YA KAMPUNI YA   HOOD LIKIENDESHWA NA
 DEREVA OMARY  SAID, MIAKA 50, MZIGUA, MKAZI WA MABIBO DSM LILIGONGANA NA GARI NO IT.3014 TOYOTA COROLLA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA DEVIS  ANAMUNDE, MIAKA 28, MZAMBIA
 MKAZI WA MUNZE LUSAKA NA KUSABABISHA KIFO CHA DEREVA HUYO 
PAPO HAPO.

 MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA MAGARI YOTE MAWILI NA DEREVA WA HOOD BUS AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHANA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

No comments:

Post a Comment