MKAZI wa Mtaa wa Mpanda Hoteli mjini Mpanda, Aloyce Sali (32) amefariki dunia baada ya kunywa pombe haramu ya gongo kupita kiasi kwa siku mbili mfululizo bila kula chakula chochote.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema kifo cha mtu huyo kilitokea juzi saa 4:30 nyumbani kwake, mtaa huo wa Mpanda Hoteli ambako alikuwa amepanga chumba.
Kwa mujibu wa kamanda, kabla ya tukio, Sali aliondoka nyumbani kwake saa 7 mchana na kwenda kilabu cha kuuza pombe za kienyeji inayomilikiwa na mtu anayetambulika kwa jina moja la Mwandosya, Mtaa wa Mpanda Hoteli.
“Alianza kunywa pombe hiyo ya gongo kwa siku mbili mfululizo bila kula chakula chochote,” alisema kamanda.
Inadaiwa alirudi nyumbani usiku na kulala. Wapangaji wenzake walipoona imefikia saa 6 mchana, walipata wasiwasi ndipo walipovunja mlango wa chumba chake na kubaini amefariki dunia.
No comments:
Post a Comment