
----------------
Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone anatarajia kuwaburudisha wakazi wa jiji la Mwanza kwenye mkesha wa Christmas, December 24.
Ben ambaye ni moja kati ya mapromota waliomsainisha Chameleone mkataba wa kupiga show hiyo amewahakikishia wakazi wa jiji hilo kuwa show hiyo itakayofanyika eneo la ufukweni (Charcoal Ribs) itakuwa ya ubora wa hali ya juu.
"Tutafunga sound mpya ya mtikisiko, tutajenga jukwaa kubwa bora tena la kisasa, tutafunga taa za kisasa pamoja na huduma nzuri kwa wateja watakaofika ufukwe wa Charcoal Ribs Mwanza, nia na madhumuni kuufanya usiku huo kuwa mkubwa, mzuri wenye mengi maajabu katika burudani" Amesema Ben.
No comments:
Post a Comment