jeri Cox Chastain akikagua baadhi ya vitu vilivyokuwamo ndani ya pochi hiyo.
Vitu visivyouzika ambavyo mwanamke mmoja alipoteza kwa zaidi ya kipindi cha miaka 20 hatimaye vimerejeshwa kwake.
Pochi ya rangi ya bluu bahari iliyoibwa Desemba, 1990 kutoka kwa Jeri Cox Chastain, mama aliyekuwa akifanya kazi mbili wakati huo, imerejeshwa katika himaya yake.
Msamaria mwema aliiona pochi hiyo katika paa la vigae vya jengo moja huko Spartanburg, South Carolina, majengo kadhaa kutoka sehemu ambako Chastain alikuwa akifanya kazi wakati huo, na kumpa kumbukumbu ya miaka kadhaa iliyopita katika mchakato huo.
Chastain anakumbukia siku hiyo, 'siku ya malipo,' kwa uwazi. Alikuwa akifanya kazi Hospitali ya Doctor's Memorial, ambayo ilifungwa mnamo mwaka 1994.
Pochi hiyo ilikuwa imeibwa wakati alipotoka ofisini kwake, kabati la chuma, kwenda kununua vitafunwa.
Wakati huo aliamini kuna mtu katika jengo la ofisi yake amemuibia fedha hizo na kisha kuitupa pochi hiyo.
"Nilihisi tu ilikuwa imetupwa kwenye pipa la taka mahali fulani."
Badala yake, Chastain alipigiwa simu kutoka polisi mapema wiki hii ikimweleza kwamba pochi hiyo aliyodhani imetoweka kabisa, imepatikana.
Shastain alikwenda kituo hicho cha polisi siku iliyofuata kuitambua pochi hiyo, ambayo ilikuwa katika 'hali safi.'
Ingawa pesa hizo zilizokuwamo, hakika, zilikwenda Shastain alifurahi kupita kiasi kuona mlolongo wa picha na kitabu cha kumbukumbu.
Ilikuwa ni picha ya kijana wake, sasa ana miaka 28, alipokuwa na miaka mitano akiwa kavalia nguo ambazo wakati fulani zilikuwa zikimilikiwa na baba yake.
Pia katika pochi hiyo kulikuwa na kadi za manunuzi na hata kadi za huduma ya matibabu kwa ajili yake na mwanae, pia cheti cha kuzaliwa cha mwanae huyo.
"Kuna mtu anawezekana kuwa alichukua [vyote hivi] na kufanya maisha mapya kwa [wao wenyewe]."
Kwa sasa Chastain ana furaha kufanya safari hii ya kumbukumbu, lakini anataka kumshukuru mtu aliyerejesha pochi yake.
Hii hakika si mara ya kwanza mtu mwaminifu kurejesha pochi iliyopotea kipindi kirefu sana.
Kutoka kwenye jengo hilo hilo, miaka michache iliyopita alirejesha pochi iliyopotea tangu mwaka 1996.
No comments:
Post a Comment