Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman aliwaeleza waandishi wa habari kuwa mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) mwenye miaka 18 alitoroshwa na diwani huyo Septemba 12 mwaka huu.
“Majira ya saa 1:30 usiku katika kitongoji cha Kibumbe kata ya Kiwira Kati, Mkulima Raphael Frank(42) na mkewe Susan (38) wakiwa nyumbani kwao waligundua mtoto wao huyo hayupo ndipo jitihada za kumtafuta zilianza bila mafanikio,” alisema Kamanda huyo.
Alisema siku iliyofuata saa 12 jioni wazazi hao walitoa taarifa polisi baada ya kuona mtoto wao hakulala nyumbani hali ambayo si kawaida.
Hata hivyo saa 3:00 usiku wa Ijumaa, mtoto huyo alirejea nyumbani na baada ya kuhojiwa na wazazi wake alijibu alikuwa kwa diwani huyo mwenye miaka 28.
“Aliwaeleza wazazi wake kuwa alilala na diwani huyo katika nyumba ya mdogo wake ambaye jina lake halijajulikana na kabla ya kukutana waliwasiliana kwa njia ya simu ya mkononi”, alisema Athuman.
Kamanda huyo alisema diwani huyo amekamatwa na upelelezi unaendelea. Kutokana na tukio hilo, Kamanda Athuman ametoa wito kwa jamii hasa wanafunzi kujiepusha na madhara ya kufanya mapenzi kwani ni hatari kwa afya zao na maisha yao ya baadaye.
SOURCE: HABARI LEO
No comments:
Post a Comment