aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, November 29, 2013

Samson Mwigamba atishia kuuanika waraka haramu wa MBOWE wenye lengo la kummaliza Zitto Kabwe...Adai kuwa CHADEMA makao makuu IMEOZA


TAARIFA YA SAMSON MWIGAMBA KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU WARAKA WA MKAKATI WA MABADILIKO 2013 

Jumatano, 27 Novemba 2013
Jana katika taarifa kwa waandishi wa habari, Mhe. Tundu Lissu na Mhe. John Mnyika waliudanganya umma kuhusu waraka unaohusu Mkakati wa Mabadiliko 2013. Katika maelezo yao waheshimiwa hawa, pamoja na mambo mengine, walidai kuwa waraka uliosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ni feki. Ukweli ni kwamba:

Ninathibitisha kwamba waraka uliosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ni sahihi neno kwa neno kama nilivyousoma katika magazeti ya HabariLeo, Jamhuri na Rai, pamoja na nakala iliyopo Jamii Forum. 

Ili kuthibitisha kwamba waraka ule ndio wenyewe, nawatumieni ‘soft copy’ kutoka kwenye kompyuta mpakato (laptop) yangu ambako ndiko ulikoibwa na viongozi wa chama baada ya kunipora kwa nguvu laptop yangu Oktoba 25 na kukaa nayo hadi jioni ya Oktoba 28.
 
 Naomba kila mtu asome neno kwa neno waraka ninaowapa leo halafu afananishe na ule uliopo kwenye magazeti na kwenye mtandao ili mjiridhishe kama kweli sio wenyewe. Kama Lissu na wenzake wana mpango wa kuuchakachua waraka huu wamekwama!

Waraka huu si wa uhaini wala mapinduzi wala usaliti kama inavyodaiwa na akina Lissu. Huu ni waraka wa kusaka ushindi katika uchaguzi halali ndani ya chama ambao ulikuwa ufanyike Desemba 2013, na ambao sasa umesogezwa mbele. 
 
Napenda ijulikane kwamba wakati wa uchaguzi si jambo la ajabu kuwa kwa wanachama kuwaunga mkono wagombea tofauti. Nimekuwa karibu na Mwenyekiti Mbowe kwa miaka mingi na ninajua kwamba yeye naye anao mkakati tena unaohusisha mbinu haramu za kuhakikisha anammaliza Zitto na yeye kupita bila kupingwa kwenye uchaguzi huo. Wanaoshiriki mkakati wake ni pamoja na Lema, Lissu na wakurugenzi kadhaa waliopo makao makuu.
 
Waraka huu ulipaswa kuwa siri ndani ya watu watatu tu (M1, M2 na M3) na haikutarajiwa kwamba ungevuja kwa jamii. 

Bahati mbaya viongozi wa chama baada ya kuunasa waraka huu kutoka kwenye komputa yangu mpakato (laptop), na baada ya kikao cha Kamati Kuu, waliamua, kwa jazba na bila kutumia busara ya kiuongozi, kuusambaza waraka huo kwenye vyombo vya habari kwa lengo la kuwakomoa na kuwadhalilisha waandaji. 

Sasa baaada ya kugundua madhara ya waraka huo machoni pa jamii wameamua kuukana. Ni ajabu kwamba wanaukana waraka ambao waliusambaza wenyewe. 
 
Nasisitiza kwamba mambo yaliyopo kwenye waraka ni bayana na dhahiri. Sibahatishi kwa sababu mimi nimefanya kazi makao makuu kama Mhasibu Mkuu hadi Mwezi Aprili 2012. 
 
Ni kwa kutambua uozo uliopo katika uongozi wa chama makao makuuniliona umuhimu wa kubadilisha uongozi kwa njia za kidemokrasia ili tukiokoe chama na hatukuwa na nia wala sababu za kuanika haya yote kwenye umma. 
 
 Kwa sababu za chuki na kukosa busara za kiuongozi huyo anayeitwa Mwanasheria Mkuu akawashauri viongozi wetu kijinga wauanike waraka mbele ya macho ya watanzania. 

Wangekuwa na akili na busara baada ya yote haya kutokea wangejiuzulu au kuitisha uchaguzi mara moja.

Tunatambua kwamba viongozi wetu wanamchukia Mheshimiwa Zitto Kabwe kwa siku nyingi sana na wametamani kumfukuza siku nyingi. 

Hata hivyo, ninawashauri watafute sababu nzuri za kumfukuza uongozi na hata uanachama kwa sababu yeye hahusiki na waraka wetu wa Mkakati wa Mabadiliko 2013 hata chembe, pamoja na kwamba yeye ndiye alikuwa na bado ndiye mlengwa mkuu, kama atakubali.

Samson Mwigamba (M3)
Arusha
Jumatano, 27 Novemba 2013

Hivi Ndivyo DIANOND Alivyowafanyia Usaili Waliotuma maombi ya Kujiunga kundi lake la WCB-WASAFI



Siku ya jana tulifanya zoezi la kuwafanyia interview baadhi ya watu waliotuma maombi yao kwa mujibu wa ,tangazo la kazi nilillolitoa juzi,mwitikio wa watu ulikuwa mkubwa,watu waliotuma email zao pamoja simu,kiasi ilituwia vigumu 
kuwataka wote waje kwenye interview,ilitubidi tuchague baadhi ya watu ambao tulihisi wanaweza kukidhi sifa tulizozihitaji ingawa nao pia tulipata changamoto ya wengi wao kuja pasipo kuzingatia maelekezo na maagizo ya tangazo lilivyotaka,hivyo jana nikishilikiana na wataalamu wa hizo sekta tulisaili na mwisho wa siku tutachukua wale wenye viwango tunavyovihitaji na kuungana na team ya WCB-WASAFI,.....
Ahsanteni sana.

Ray, Chuchu Hans sasa sio siri tena...walianika Penzi lao hadharani...!!

 
AMA kweli penzi ni kikohozi kulificha huwezi! Hatimaye uliokuwa uhusiano wa chini kwa chini wa nyota wawili wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans, siyo siri tena baada ya wahusika hao wakuu kujiachia ‘live’.

KIMAHABA ZAIDI
Ishu hiyo ilitokea mapema wiki hii ambapo Chuchu alitundika picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na Ray chumbani kimahaba.

Kufuatia tukio hilo kuliibuka gumzo kubwa na kulifanya jambo hilo kuwa ndiyo habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa wa filamu za Kibongo.
Katika picha hiyo, Chuchu anayetumia jina la Chukichuku kwenye Instagram aliambatanisha na maneno yaliyosomeka ‘Me n U’ akimaanisha yeye na Ray hivyo kutoa fursa kwa mashabiki wao kusema chochote.

Kwa mujibu wa mashabiki hao, Ray na Chuchu kwa sasa ndiyo love bird au ‘maua’ yanayopendezesha tasnia hiyo.
“Mmependezaaa…mapenzi waziwazi,” ilisomeka komenti ya mmoja wa mashabiki hao.
“Nilikuwa simuelewi Ray lakini hapa nimemsoma. Wamependeza sana,” ilisomeka komenti nyingine iliyoungwa mkono na mashabiki wengi kwa kupata ‘likes’ nyingi.

Mwingine aliandika: “Sasa walichokuwa wanagombea Mainda (Ruth Suka) na Johari (Blandina Chagula) kipo wapi? Ona sasa wamekosa wote… hahahaaa… wawaache miaka isiyohesabika.”

HAKUNA KIFICHO TENA
Katika kunogesha mambo, baadaye Chuchu aliweka picha ya Ray akimsifia jambo lililodhihirisha kuwa kwa sasa hawafanyi tena kificho kama miezi kadhaa iliyopita.

Habari za chini ya kapeti kutoka kwa wasanii wenzao wanaokuwa nao lokesheni zilieleza kuwa wawili hao wamekuwa wakionesha waziwazi kuwa wao ni item (kitu kimoja).
“Kuna siku tulikuwa tuna-shoot maeneo ya Sinza-Mori (Dar), yaani ungewaona wala usingeuliza maana kama hujui kusoma, ungeangalia hata picha. Yaani mapenzi kama njiwa!
 
“Sasa hivi ndiyo uhusiano ambao upo ‘hoti’ kwenye tasnia yetu, sema ndiyo hivyo wenyewe walikuwa hawapendi ijulikane lakini naona wameshindwa kuendelea kujificha,” alisema mwigizaji huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini.

CHUCHU ATAKA WASIINGILIWE
Baada ya kujikusanyia data, Ijumaa lilimtafuta Chuchu akiwa mmoja wa wahusika wakuu ambapo alipopatikana alikuwa na haya ya kusema: “Hayo ni mambo yetu binafsi, naomba tusiingiliwe katika mambo yetu.”


Ijumaa: Chuchu wewe ni kioo cha jamii na mashabiki wako wanataka kujua ukweli juu ya uhusiano wako na Ray. Unalizungumziaje hilo?
Chuchu: Weweee…sikia! Nimeshasema sitaki mtu aniingilie mambo yangu. Kwani mnataka nini nyiye?

Ijumaa: Je, hiyo picha mliyopiga chumbani ni hotelini au nyumbani?
Chuchu: Siwezi kukuelezea tumepiga wapi, iwe hotelini au nyumbani haiwahusu, naomba mniache jamani mbona hivyo? Kwani vipi? (kisha akakata simu).

KAKA MKUBWA VIPI?
Jitihada za kumpata Ray ‘Kaka Mkubwa’ katika tasnia ya filamu za Kibongo ili kupata neno lake juu ya ishu hiyo ziligonga mwamba baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa na hata alipofuatwa ofisini kwake, RJ Productions pale Sinza-Mori, Dar hakupatikana.
KABLA YA PICHA
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai mazito kuwa Ray na Chuchu wanatoka lakini habari hizo zilikosa mashiko kwa kuwa hakukuwa na ushahidi wowote.
 
Ilidaiwa kuwa hata ile vita ya hivi karibuni ambapo Johari na Chuchu walizichapa kavukavu ilitokana na kugombea penzi la Ray.
JOHARI ASARENDA
Hata hivyo, baadaye Johari alinyoosha mikono kuashiria ‘kusarenda’ na kumwachia Chuchu atawale ulingo ambao ulimshinda pia Mainda.

Ilidaiwa kuwa katika kutekeleza kile walichokiita mpango wa siri, Chuchu na Ray waliunda kampuni yao na kuipa jina la kolabo la Chura wakimaanisha Chuchu na Ray.

TATIZO KUBWA
Wakati hayo yakiendelea, taarifa rasmi ni kwamba bado Chuchu ni mke wa ndoa wa bosi wa Kampuni ya 2 Eyez Productions, Frank Mtao anayeishi ughaibuni huko Australia akiwa ni mwenyekiti wa Wabongo waishio pande hizo.


Mbali na kuwa mke wa mtu, pia Chuchu ni mama wa watoto wawili hivyo uhusiano wake tata na Ray unalenga kuzalisha tatizo kubwa kwenye ndoa ya Chuchu ikiwa ni miezi kadhaa tangu wawili hao walipodaiwa kufumaniwa na mwanaume mwingine wa Chuchu.

Source: Gazeti  la  Ijumaa

Mpasuko waendelea Kuitafuna CHADEMA....sasa kamati kuu yagawanyika Makundi mawili..!!

BAADA ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kufunga mjadala wa mgogoro unaoendelea ndani ya chama hicho, agizo hilo limeonekana kufuatwa vema na wajumbe wa Kamati Kuu, lakini limewafungua wajumbe wa Baraza Kuu, Mkutano Mkuu na taasisi za chama hicho.
 
Tayari imeripotiwa kuwa uamuzi wa chama hicho kumvua madaraka aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto na aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo, umeipasua Kamati hiyo katika vipande vya wafuasi wa wagombea uenyekiti wa chama hicho katika uchaguzi ujao, Mwenyekiti wa sasa Taifa, Freeman Mbowe na Zitto.

Miongoni mwa wajumbe wa Kamati Kuu wanaotajwa kumwunga mkono Mbowe ni Dk Slaa, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu, Msemaji wa Chama hicho, John Mnyika na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Waliojitokeza waziwazi kumwunga mkono Zitto ni Dk Mkumbo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba ambao kwa hatua hiyo wamevuliwa nyadhifa zao na aliyekuwa Mwanasheria wa Mbowe, Albert Msando ambaye sasa ni Mwanasheria wa akina Zitto.

Wengine wanaotajwa kumwunga mkono Zitto ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti , Said Arfi ambaye uamuzi wa kumvua Zitto madaraka, ulisababisha ajiuzulu nafasi hiyo.

Hata hivyo, Profesa Mwesiga Baregu, ameripotiwa kukionya chama kwa hatua hiyo, akisisitiza kuwa baada ya uamuzi huo wa Kamati Kuu dhidi ya Zitto, chama kilitakiwa kisubiri baraka za Baraza Kuu, ndipo uamuzi huo utangazwe.

Wafuasi Baraza Kuu Jana Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Temeke na mjumbe wa Baraza Kuu, Patrick Joseph, alitoa kauli iliyodhihirisha kuwa yeye ni mmoja wa wanaomwunga mkono Zitto.

Joseph katika kauli yake, alionekana kuungana na Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Geita, Abdalah Hamis, ambaye hakumung’unya maneno, kwani aliweka wazi kuwa yeye atamwunga mkono Zitto. Mwenyekiti huyo wa Temeke, aliitisha mkutano na waandishi wa habari akimtaka Mbowe, kuitisha mkutano wa dharura wa Baraza Kuu, ili litoe uamuzi sahihi kuhusu Zitto na wenzake.

Pamoja na kuwa yeye si mjumbe wa Sekretarieti ya chama, inayopanga ajenda za Baraza Kuu, Joseph alisema ajenda ya kikao cha Baraza hilo, ni kutaka viongozi wawaeleze wajumbe kwa nini wamesambaza waraka wanaodhani unawadhalilisha Zitto, Dk Mkumbo na Mwigamba, wakati waraka huo umekidhalilisha chama kwa kuonesha udhaifu wa Mwenyekiti na Katibu Mkuu.

Akionekana kuwasemea wajumbe wenzake wa Baraza hilo, Joseph alisema katika mkutano huo, wajumbe watataka waelezwe kwa nini wasiamini kwamba uamuzi huo umeathiriwa na hofu ya uchaguzi wa ndani wa chama.

Pia watataka sababu zilizoifanya Sekretarieti ya Kamati Kuu, itangaze ratiba ya uchaguzi mkuu wa ndani, baada ya kuwachafua miongoni mwa watu waliotarajiwa kugombea nafasi, mpaka kuwavua uanachama.

Mjumbe huyo bila kuonesha hofu ya kuvuliwa madaraka kama wenzake walivyofanyiwa, alisema umefika wakati wa kuijenga Chadema bila kufuata masuala ya ubaguzi wa kidini, kikabila ama kikanda kama ambavyo inajulikana nje. 

Akifafanua hoja hiyo ya ubaguzi, alisema kuwapo kwa Zitto na Arfi katika nafasi za viongozi wa kitaifa, ilikuwa ni ishara ya kutokuwa na udini ndani ya chama.

"Sasa inawezaje kuwatimua na kuwaita wasaliti watu ambao mmekuwa mkijivunia kuwa ni ishara kwamba hakuna udini?"
Alihoji Mwenyekiti huyo wa Chadema Temeke, na kusisitiza kuwa hayuko tayari kuburuzwa wala kuruhusu baadhi ya viongozi waendelee kuibomoa demokrasia wanayoitangaza kila kukicha.

Joseph alisema chama chao kimekuwa na tabia ya kuingia kwenye migogoro kila kinapokaribia kwenye uchaguzi wa ndani hali inayosababisha kuchafuana na kutukanana miongoni mwa viongozi kwa kuitana wahaini na wasaliti.
Alisema amefadhaishwa na uamuzi wa Kamati Kuu dhidi ya Zitto na Dk Mkumbo, kwani haikuwa na mamlaka ya kikanuni wala kikatiba kufanya hivyo na kuutangaza kwa umma.

Kauli hiyo ya Joseph, ilitolewa pia na Dk Mkumbo, Msando ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu na Profesa Baregu. Hata hivyo, imekuwa ikipingwa na Lissu kwa kutumia Katiba hiyo hiyo ya Chadema, kwamba kuna kipengele kiliongezwa katika Katiba ya sasa, kinachoruhusu Kamati Kuu kuchukua uamuzi kama huo inapoona inafaa.

Joseph alisisitiza kuwa haingii akilini chama kinachopanga mikakati ya kushika Dola, kifukuze na kuogopa watu wanaopanga mikakati ya wao kushinda uchaguzi ndani ya chama.

"Kama ni kweli kupanga mikakati ya uchaguzi ndani ya chama ni uhaini na usaliti, basi operesheni zetu za chama ikiwemo ya M4C zenyewe zinapaswa kuwa uhaini uliopitiliza kwa kuwa nayo ni mikakati ya chama kushika Dola," alisema Patrick. Mikoani Juzi Katibu wa Mkoa wa Geita, Hamis alitamka:

“Nikiwa Katibu wa Chadema, Mkoa wa Geita nasema mimi na wenzangu pia wote ndani ya mkoa wetu tutakuwa nyuma ya Zitto. Nyakati za uonevu, manung'uniko na kubaguliwa sababu tu za eneo, ukanda, udini na kuchaguliana marafiki zimekwisha.”

Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Tanga, Harid Rashid, ambaye alifuatana na mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Hussein Baruti na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya Tanga, Mohamed Aufi, aliripotiwa kusema hakubaliani na uamuzi wa Kamati Kuu.

Rashid alisema Kamati Kuu ilikuwa na njia nyingi za kulipatia ufumbuzi jambo hilo badala ya kuwavua uongozi. Alisema wameamua kuwa wazi kuhusu tukio hilo kutokana na ukweli kuwa Zitto ni mtu muhimu katika uongozi wa chama.

Kundi la vijana wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Zitto jijini Mbeya nao wanadaiwa kurushiana makonde na viongozi wa Chadema katika ofisi ya chama hicho Mbeya Mjini kwa madai ya kutofautiana misimamo kuhusu uamuzi wa Kamati Kuu. Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Mbeya Mjini, David Mwambigija ‘Mzee wa Upako’, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo juzi mchana.

Mjadala wafungwa Kudhihirisha kuwa wajumbe wa Kamati Kuu wametii agizo la Dk Slaa la kufunga mjadala huo, jana gazeti hili lilipotafuta namna ya kumpata Mwigamba, alikuwa akikata simu zake.

Lilipomtafuta Profesa Baregu, alipokea lakini alijibu kwa ufupi kwamba kwa sasa hawezi kuzungumzia mambo ya Chadema. Wafuasi wa Mbowe Baada ya Zitto na Dk Mkumbo kuzungumza baada kuvuliwa madaraka, Mnyika na Lissu waliitisha mkutano na waandishi wa habari kukanusha yote yaliyozungumzwa.

Katika mkutano wao akina Mnyika, walidai kuwa waraka uliochapishwa na magazeti kuwa ndio uliomponza Zitto kwa kuwa si uliowasilishwa mbele ya Kamati Kuu.

Lakini mwandishi wa waraka huo, Mwigamba alijibu haraka kuwa hakuna kilichohaririwa bali waraka huo ndio sahihi. Kutokana na vurugu zilizotokea Kigoma, wafuasi wa Mbowe walisema ni za kutengeneza na leo wamejipanga kufanya mkutano kutetea hoja kuwa Kigoma anakotoka Zitto, wanaunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu.

Mbali na kikao hicho cha Kigoma, pia Mratibu Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (Chasso), Dar es Salaam, Elihuruma Himida, alisema leo umoja huo utatoa kauli kupinga matamko ya wanaojiita wanafunzi wa vyuo vikuu, waliosema watazunguka nchi nzima kumwunga mkono Zitto.

Elihuruma pia alidai kuwa mkutano wa Zitto kujibu hoja za kuvuliwa madaraka, uliandaliwa na wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), akina Juliana Shonza, waliohudhuria mkutano huo wa Zitto, huku viongozi wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), wakizuiwa kumsikiliza kiongozi huyo.

----Habari Leo

Kapuya hakamatiki....atua Bongo kwa mbwembwe kibao, polisi wamgwaya....!!


HATIMA ya Mbunge wa Urambo Magharibi Juma Kapuya (CCM), anayetuhumiwa kutishia kumuua binti anayedaiwa kumbaka, amerejea nchini jana akitokea nchini Sweden, huku Jeshi la Polisi likikwama kumtia mbaroni kama lilivyokuwa likitamba. 
 
Wakati mbunge huyo akiwasili nchini na kupokewa na kusindikizwa na wapambe wake, Bunge limeridhia kukamatwa kwake kwani tuhuma zinazomkabili ni za jinai na zinamhusu yeye binafsi.
 
Mbunge huyo ambaye amepata kuwa waziri, amerejea nchini jana majira ya saa tano asubuhi kwa ndege ya Shirika la Qatar na kutua katika uwanja huo wa ndege na kuondoka kupitia mlango wa watu maarufu (VIP).
 
Habari zinasema mbunge huyo alipoondoka katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere alikwenda moja kwa moja kwenye moja ya hoteli za jijini Dar es Salaam na kuacha mizigo yake, kisha kuondoka na gari namba T 104 AEZ Toyota, huku wapambe wake wakiwa katika gari namba T 170 BGY aina ya Benz.
 
Wakati Kapuya akitua katika uwanja huo wa ndege, polisi ambao kwa takriban wiki moja sasa wamekuwa wakitamba kutaka kumtia mbaroni mara baada ya kutua, baadhi yao walionekana wakisalimiana naye kama vile hawakuwa wanamuwinda.
 
Tangu Profesa Kapuya alipoondoka nchini huku akizongwa na kashfa ya kutishia kumuua binti anayedaiwa kumbaka, polisi wamekuwa wakitamba kutaka kumtia mbaroni na kuahidi kuwa mara baada ya kurejea nchini mbunge huyo angekuwa chini ya ulinzi.
 
Tanzania Daima juzi liliripoti mkakati wa polisi kutaka kumtia mbaroni mbunge huyo mara atakapotua kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 
Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zilisema kuwa kumekuwa na shinikizo kutoka ndani na nje ya jeshi hilo kutaka waziri huyo wa zamani ahojiwe kuhusiana na tuhuma zinazomkabili za kutishia kumuua binti anayedaiwa kumbaka.
 
Hatua ya polisi kutaka kumnasa Kapuya akiwa uwanja wa ndege inadaiwa kuchangiwa na taarifa ya  wiki iliyopita kwamba baadhi ya vigogo wa jeshi hilo walishiriki kufanikisha safari ya mbunge huyo nje ya nchi huku wakijua fika anatakiwa na polisi.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alipoulizwa kuhusu ujio wa Kapuya na kisha kuendelea kuachiwa huru, alisema yuko nje ya Jiji la Dar es Salaam na hakuwa na taarifa za kurejea kwake.
 
Hata hivyo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Yusuph Mrefu, alipoulizwa kuhusu sakata la Kapuya, alisema hakuwa na taarifa ya kile kinachoendelea, kwa kuwa ndiyo kwanza amekabidhiwa ofisi.
 
“Mimi niambie jambo jipya, hapa ofisini ndiyo leo nimeingia kukaimu, sasa hayo mambo nitayajulia wapi, ni vema ungeniambia jambo jipya tuweze kutatua,” alisema Mrefu.
 
Kwa upande wake, Bunge limesema kuwa sakata la Profesa Kapuya lilifikishwa bungeni na kubaini kuwa ni la jinai, hivyo linapaswa kwenda kwenye mkondo wa kisheria.
 
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila, alithibitisha kulifahamu suala hili, kwani binti aliyedai kubakwa na kutishiwa kuuawa na mbunge huyo alikwenda bungeni wakati Bunge la 13 lilipokuwa likiendelea mjini Dodoma.
 
“Suala la binti huyo lilifikishwa ofisini kwangu kupitia kwa msaidizi wangu ambaye  alisikiliza hoja na rai yake na kushauriwa kuwa hilo ni suala la jinai na linapaswa liende katika mkondo wa kisheria, hata hivyo binti huyo alitambulishwa kwa Spika kama kiongozi wa wabunge na kuelekeza kuwa tumshauri alifikishe katika mamlaka husika,” alisema Kashilila.
 
Tayari binti anayedaiwa kubakwa na kutishiwa kuuawa ameshafungua jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam na Jeshi la Polisi likaahidi kumkamata Kapuya popote alipo ili kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.
 

Tayari makachero wa polisi wameanza kufuatilia namba ya simu inayodaiwa kutumika kumtisha binti huyo na wakati mwingine kutumika kurusha pesa kwa njia ya mtandao, zinazodaiwa kutoka kwa Profesa Kapuya kwenda kwa binti huyo.

Credit-Tanzania Daima

Laana!! Mke Aishi na wanaume wawili ndani ya Nyumba Moja, Mmoja ni Mume wa Ndoa na Mwingine ni hawara huko Kigogo-Mburahati...!!

DUNIA ina kila kituko, kama hujawahi kukisikia omba Mungu akupe uzima!  Mama mmoja, aitwae  Elizabeth Selestine, mkazi wa Kigogo-Mburahati, Dar hivi karibuni alizua timbwili nyumbani kwake baada ya majirani, wajumbe na ndugu zake kumjia juu kwa kitendo chake cha kuishi na wanaume wawili kwenye chumba kimoja, Ijumaa lina mkasa kamili. 
Elizabeth Selestine anayeishi na wanaume wawili.


Ndani ya timbwili hilo, watu kibao walikuwepo, lakini muhimu sana ni mdogo wa mwanamke huyo, Oscar Selestine (17) ambaye alianika kila kitu.
Oscar alisema shemejiye anaitwa Benedicto Ludovic na dada yake huyo walipanga kwenye nyumba ya akina Juma Ngulumo ambaye ndiye mwanaume wa pili, yaani hawara.

 
Mume wa ndoa.


“Baada ya kuanzisha uhusiano na Juma, mwenye nyumba (baba wa Juma) aliwafukuza akiogopa kuwa kwa tabia ya dada lisije likatokea balaa kubwa. Hata mimi na mdogo wangu tuliishi kwa dada na shemeji.
“Dada na shemeji  wakahamia kwenye chumba kimoja nyumba ya jirani, dada akaniambia mimi na mdogo wangu mwingine tuishi nao huku tukitafuta pa kulala kwa sababu wao walipata chumba kimoja ambacho tulikuwa tunalala wote, mimi, mdogo wangu, dada, shemeji na watoto wao wawili.

Lakini siku moja nilishangaa kumwona Juma akija na godoro hapo hapo kwenye chumba kimoja huku shemeji akiwemo,” alisema Oscar na kuwashangaza hata mapaparazi. Dunia ina mambo mengi.
 
Mama mwenye nyumba.


 “Nilishtuka sana! Kulala kwenyewe, shemeji  na dada kitandani, Juma akawa analala chini wakati na yeye ni mtu mzima tena ana watoto,” alisema Oscar.
Oscar aliendelea kusema kuwa, siku moja alishangaa kumwona Juma akimpiga dada yake, alipojaribu kuuliza dada huyo  akamjibu: “We mtoto, hayakuhusu.” Mwisho yeye na mdogo wake wakafukuzwa na kuambiwa wasifike  nyumbani hapo.
Oscar hakuona sababu ya kufunga kinywa bila kumalizia kusema yote, akaanika kwamba ilifika mahali Juma alianza kumpiga shemeji yao kisa eti amekuwa na wivu kwa mke wake. Makubwa hayo!

Kumbe mtoto mmoja wa dada alikuwa akiona kila kitu, siku moja akaanika siri kwamba, Juma huwa anampiga shemeji usiku na ili amuache dada alale naye chini,” alisema Oscar.
 
Ndugu wa mke.


Oscar akasema hakuna siri ya watu wawili, baadaye habari zilizagaa kwa ndugu wote kuwa dada yao anaishi na wanaume wawili, ndipo mama mwenye nyumba alimuita na kumkanya lakini hakusikia.
Mwenye nyumba alipoona jeuri hiyo alimuita tena na kumpa siku saba aondoke ndani ya nyumba yake lakini bado Elizabeth hakufanya hivyo.
Oscar tena: “Huwezi amini ilifika wakati shemeji akileta chakula kinapikwa halafu yeye hatengewi, anatengewa Juma, shemeji akiuliza anaambiwa akale na watoto. Sisi hatumuelewi shemeji, kama ni madawa basi yamemkolea sana.

Ikadokezwa kwamba tukio hilo lilifika mbali, hadi kwa  wazazi wa mwanaume, Kilosa, Morogoro ambao walifunga safari mpaka Dar lengo lilikuwa kuwachukua wajukuu na mtoto wao Benedicto, lakini ilishindikana kwani waliambulia kutukanwa na mwanamke huyo, wakaondoka wakiacha laana nyuma.
Vituko viliendelea siku hadi siku, siku moja Benedicto au maarufu kwa jina la ‘baba Gire’ alikwenda kwa mjumbe wa eneo hilo, Maua Thabiti  huku akilia na kuapa ipo siku atafanya kitu kibaya ambacho mkewe na Juma hawatakaa wakisahau.
Mjumbe huyo ambaye ni wa shina namba 48, mtaa wa National Housing Mburahati, Dar alikiri kupokea malalamiko hayo lakini akasema mwanaume huyo anaogopa kuweka wazi kwa sababu atapigwa, hivyo anamuachia Mungu.

Mwenye nyumba wanayoishi watu hao, Flora Mtumbati alipoulizwa naye alikiri kuwa, Eliza anaishi na wanaume wawili.
“Baada ya kubaini hilo, Eliza aliitwa na Jumuiya ya Katoliki anakosali na kuonywa. Mimi nilimpa siku saba za kumtoa Juma na kubaki na mumewe, aliniahidi lakini hakufanya hivyo, bora watu wa magazeti mmekuja mnaweza kunisaidia,” alisema Flora.
Baada ya kuongea na vyanzo vyote, gazeti lilimtafuta Elizabeth:

Huyu bwana (Juma) alikuja kwangu kwa matatizo, alikaribishwa na mume wangu, nilimkaribisha chumbani kwangu kwa sababu ndiyo chumba hichohicho. Hata hivyo, leo (Ijumaa iliyopita) anahama.”
Baada ya waandishi kuondoka, mwanamke huyo alitishia kujiua. Siku ya pili, waandishi waliambiwa kuwa mwanamke huyo alikimbilia Kimara  kwa wifi yake ambaye ni ndugu wa Juma.

Benedicto alipopatikana alisema: “Sikuamini kama mke wangu anatembea na Juma ingawa niliwahi kusikia. Kuhusu kupigwa ni kweli hasa akilewa pombe. Baada ya sakata hili mke wangu amesema kwa watu kuwa hata mtoto wa mwisho si wangu, ni wa Juma. Inauma sana.”
Baada ya waandishi kuibua ishu na watu kujaa, inadaiwa  Juma alitafuta vijana na kumpa kichapo cha nguvu baba Gire ambapo ameshonwa nyuzi kumi na mbili mdomoni na jichoni.
Kesi hii ilifikishwa Kituo cha Polisi Mburahati na kufunguliwa jalada namba MBR/RB/1204/13  KUJERUHI.



---Gpl

Thursday, November 28, 2013

Watanzania wawili wanaswa na Shehena ya Kilo 55 za madawa ya Kulevya huko Afrika Kusini...!!



Johannesburg/Dar. 
 Watanzania wawili wanahojiwa na Polisi wa Afrika Kusini baada ya kukamatwa jana na kilo 55 za dawa za kulevya.
Watu hao wawili wanatazamiwa kufikishwa mahakamani kesho kujibu tuhuma za kukamatwa na dawa hizo zenye thamani ya Rand75 milioni (Sh11.7 bilioni).
Maofisa wa Kikosi Maalumu cha Kupambana na Makosa ya Jinai na Rushwa cha Afrika Kusini (The Hawks), kiliwakamata watu hao katika Kitongoji cha Kempton Park, Ekurhuleni, Jimbo la Gauteng.
Msemaji wa Hawks, Paul Ramaloko alisema jana kuwa maofisa hao walivamia nyumba waliyokuwa wanaishi Watanzania hao na kukuta mzigo huo.

Hata hivyo, alikataa kutaja majina ya watu hao kwa kuhofia kuharibu uchunguzi akisema bado walikuwa wanawasaka watuhumiwa zaidi wakiwamo raia wa Afrika Kusini.
Alisema kikosi chao kimepata mafanikio makubwa kwa kukamata dawa nyingi kiasi hicho... “Tunakaribia kuwakamata vinara wa biashara hiyo, maana tumeelezwa kuna kundi kubwa la watu wazito,” alisema Ramaloko. Hii inakuwa mara ya pili katika kipindi cha miezi minne kwa Watanzania kutuhumiwa kubeba dawa hizo.
Julai mwaka huu, wasanii wawili Agness Gerald `Masogange’ na Melissa Edward walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo, Johannesburg wakiwa na kilo 180 za kemikali aina ya ephedrine zenye thamani ya Sh7 bilioni.
Baada ya kukaa miezi miwili jela, Masogange alipatikana na hatia ya kuingiza kemikali hiyo, ambayo hutumika kutengeneza dawa za kulevya na kutozwa faini ya Rand 15,000 (Sh2.3 milioni).
Melissa aliachiwa huru baada ya kuonekana hana hatia.
Wasafirishaji sasa watumia samaki
Katika hatua nyingine, wasafirishaji wa dawa za kulevya inasemekana wamebuni mbinu mpya ya kutumia samaki kusafirisha bidhaa hiyo haramu.

Akizungumza jana wakati wa uteketezaji wa dawa za kulevya, Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Godfrey Nzowa alisema wanatumia samaki kwa kuwa wana harufu kali.

----Mwananchi