aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, November 1, 2013

MAHAKAMA YAWATUPA JELA MIEZI 12 MASHABIKI WA MBEYA CITY WALIOLETA VURUGU SIKU YA MECHI DHIDI YA PRISONS..!!



MAHAKAMA ya mwanzo, mjini Mbeya, leo imewahukumu kifungo cha miezi 12 kwenda jela au kulipa faini ya sh.300,000 kila mmoja, watu watano kati ya sita walioshitakiwa kwa kosa la kuharibu mali katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons

KINGWALLAH AITIKISA CCM KWA KUKSUANYA SAINI ZA KUNG'OA SPIKA MAKINDA BUNGENI....MAKINDA AJIBU MAPIGO KWA KUDAI KUWA HAOGOPI LOLOTE..!!

Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema hatishwi na mchakato wa kumng’oa katika nafasi yake ambao umeanzishwa na Mbunge wa Nzega,Dk. Khamis Kigwangalla kutokana na tuhuma za kukiuka kanuni za Bunge.
 
Kadhalika Spika Makinda amepuuza hoja za Dk Kigwangalla akisema kuwa yeye hajavunja kanuni yoyote, lakini akaweka bayana kuwa mbunge huyo wa Nzega ana haki kwa mujibu wa Kanuni za Bunge kuendelea na kile anachokifanya.

Kanuni si zinamruhusu, utaratibu upo kwenye kanuni za Bunge kwa hiyo aendelee na mchakato lakini mimi ninachosema sitetereki maana hakuna kanuni yoyote ambayo nimeivunja,” alisema Makinda katika mahojiano maalumu na Mwananchi ofisini kwake jana.

Wakati Spika akitoa kauli hiyo, jana, Dk Kigwangalla alianza harakati zake za kukusanya saini za wabunge, akitafuta kuungwa mkono katika hoja ya kutokuwa na imani naye kwa madai kwamba amekuwa akikiuka kanuni.

Miongoni mwa madai ya Dk Kigwangalla ni hatua ya Makinda kufanya uteuzi wa Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, tofauti na kanuni zinazotaja wenyeviti kuchaguliwa na wajumbe wa kamati.

Hoja nyingine ni kamati hiyo ya bajeti kulipwa posho ya Sh430,000 wakati wajumbe wa kamati nyingine wamekuwa wakipewa Sh130,000 pamoja na kumteua Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba kuingia katika kamati hiyo ya bajeti wakati mbunge huyo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu.

Jana Dk Kigwangalla aliwasilisha hoja yake kwa Katibu wa Bunge na kuongeza madai mapya yakiwamo ya kuagiza kwa mabavu majedwali ya mabadiliko ya sheria kwenda kwenye kamati ya bajeti, kuvunja masharti ya kanuni ya 48 inayotoa maelekezo ya namna ya kuwasilisha na kujadili jambo la dharura na kutumia madaraka yake vibaya kwa kuvunja masharti ya Sheria ya The National Assembly (Administration) Act (Cap.115) ya mwaka 2008.

Makinda akijibu hoja hizo jana alisema alifanya uteuzi wa Chenge kuongoza Kamati ya Bajeti kwa sababu kamati hiyo ni mpya na haikuwapo katika kamati za awali, hivyo ni wazo ambalo lilitokana na mawazo ya Bunge la sasa.

Tulikuwa tunafikiria jinsi Bunge linavyoweza kuisadia Serikali ipate vyanzo vipya vya mapato. Kwa hiyo tumehitimisha wazo hili kwa kuamua kuwa na Kamati ya Bajeti. Kamati hii haikuwapo na wala utaratibu wake wa kikanuni haukuwapo. Niliamua na kanuni zinanipa uwezo huo kwamba niteue mtu ambaye ninaamini anaweza kuisimamia katika hatua za mwanzo ili tuone uzoefu utatufikisha wapi,” alisema Makinda na kuongeza:

Kamati hii hata Serikali ilikuwa haikubaliani na sisi, lakini katika muda mfupi wa utendaji wake umefanya kazi kubwa na kama tusingekuwa na Mzee Chenge ambaye ni mzoefu na anafahamu vizuri utendaji wa Serikali basi tungeshindwa na mimi siko tayari kuanzisha kitu halafu nikashindwa”.

Kuhusu posho, Spika aliungana na kauli ya Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah kwamba si wakati wote Kamati ya Bajeti imekuwa ikipewa malipo zaidi, bali ni pale tu wanapofanya kazi nje ya siku na saa za kazi tena kwa kibali chake.

Lazima walete maombi na waeleze kwa nini wanapaswa kufanya kazi kwa muda wa ziada au siku za mapumziko na mimi nikisharidhia basi wanalipwa mara mbili ya viwango vya kawaida na hiyo ni kwa mujibu wa taratibu na Kanuni zetu,” alisema.



-----MWANANCHI

ANGALIA HAPA VIDEO YA VURUGU ZILIZOTOKEA JANA UWANJA WA TAIFA...VITI ZAIDI YA 50 VYAVUNJWA..!!

1  
October 31 2013 kulikua na mechi ya Simba vs Kagera Sugar kwenye uwanja wa taifa ambapo timu hizo zilitoka 1-1 huku goli lililoleta malalamiko likiwa ni la Kagera Sugar ambalo lilifungwa kwa njia ya penat. 
Kocha wa Kagera Sugar amesifia maamuzi ya refa na kusema ‘nafurahi timu imesawazisha kwenye dakika za mwisho na refa amefanya kazi yake kwa sababu ni siku nyingi sana marefa hawagawi penat kama hizo, timu nzuri inacheza mpaka goli’ 

Kocha Kibaden wa Simba kasema ‘nashukuru tumemaliza mpira salama na vijana wametoka salama, sijafurahishwa na jinsi mpira ulivyochezeshwa, sitaki kusema hayo kwa sababu watu wana macho na wanaweza kukosoa lakini uamuzi haukuwa sawasawa, kama tutaendelea na mpira wa aina hii nafikiri tutaondoka kwenye mwelekeo…  
naomba TFF mpya iliyokuja ijaribu kutazama watu wapumbavu wa aina hii wanaokuja pale kuwaudhi watu, sijafurahishwa na mpira ulivyochezeshwa mwanzo hadi mwisho na nilijua kitatokea nini’

BABA KANUMBA AMPIGA MARUFUKU MAMA KANUMBA KUTUMIA JINA LA KANUMBA KWA NAMNA YOYOTE ILE.

Bi. Flora Mtegoa.
Katika hali ya kushangaza, baba wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba amempiga marufuku mama mzazi wa msanii huyo, Flora Mtegoa kutumia jina la Kanumba kwa namna yoyote.
Mzee Charles Kanumba.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni baba Kanumba alisema mama Kanumba hana mamlaka ya kulitumia jina la Kanumba kwani hana uhusiano nalo.
“Mimi ndiye mwenye mamlaka na jina la Kanumba kwa sababu ni la kwangu lakini namshangaa mama Kanumba kuendelea kulitumia jina hilo hata kwa watoto wasionihusu kama mtoto wa mwanaye aliyezaliwa hivi karibuni na kuitwa Kanumba Junior.

“Anahusiana nini na hilo jina wakati huyo siyo damu yangu, yeye ana baba yake kwa nini asitumie jina lake, sitaki kabisa atumie jina langu mwanangu ameshafariki na mimi ndiye mwenye mamlaka ya kutumia hilo jina,” alisema mzee huyo.
Akilizungumzia suala hiyo, mama Kanumba alisema: Sitaki kumsikia kabisa,kama vipi aende mahakamani.”

VIWANGO VIPYA VYA ALAMA ZA UFAULU ELIMU YA SEKONDARI HIVI HAPA.SASA MPAKA DIVISION 5


Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya upangaji wa viwango vya alama, matumizi ya alama endelevu ya mwanafunzi na ufaulu jana jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishna wa Elimu Profesa Eustella Bhalasesa. Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome (hayupo pichani). Waandishi wa habari na maafisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome(hayupo pichani). Picha zote na Eliphace Marwa (MAELEZO).
----
UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA, MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI NA UFAULU 
UTANGULIZI
Wizara imekusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na Matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment ama CA) kwa ajili ya kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi. Maoni ya wadau yamekusanywa kwa sababu kwa muda mrefu sasa upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika na utaratibu wake katika mitihani ya kuhitimu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita umekuwa haufanani pamoja na kwamba mitihani hiyo yote ni ya elimu ya sekondari.
 
Pia mfumo masuala mbalimbali ya mitihani katika elimu ya sekondari umekuwa na miundo tofauti ikiwemo ule unaotumika shuleni na ule wa Baraza la Mitihani la Taifa. Kwa sasa kuna miundo mikuu miwili katika mfumo huo.
 
Muundo wa Kwanza ni upangaji wa viwango katika ngazi ya Shule ambapo Alama Mgando (Fixed Grade Ranges) zifuatazo hutumika kupanga madaraja: A = 81 – 100; B = 61 – 80; C = 41 – 60; D = 21 – 40 na F = 0 – 20. Muundo huu umetumika kwa muda mrefu na umezoeleka kwa walimu na wanafunzi wa elimu ya sekondari kwa ujumla.
 
Muundo wa Pili ni wa viwango vinavyotumiwa na Baraza la Mitihani la Taifa ambapo ambapo kabla ya mwaka 2012 muundo wa viwango nyumbufu (flexible grade ranges) ulitumika. Katika muundo huu uwigo wa alama ulibadilika badilika kulingana na hali ya matokeo ilivyokuwa kwa mwaka husika. Lakini kuanzia mwaka 2012, Serikali iliamua kutumia mfumo wa Upangaji wa Alama Mgando (Fixed Grade Range) kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita. Katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 Baraza lilitumia mfumo huu wa alama mgando ambapo: A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49, F = 0 – 34. Kwa upande wa Kidato cha Sita Baraza lilitumia mfumo wa A = 80 – 100; B = 75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E = 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 – 39. Mifumo hii ya Baraza haikuwa inafahamika kwa wadau na hivyo kuwa sehemu ya malalamiko katika sekta ya elimu na mafunzo.
 
Vilevile, Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, Alama za CA zitachangia asilimia hamsini (50%) na Mtihani wa mwisho utachangia asilimia hamsini (50%). Kwa upande wa Zanzibar, CA zimekuwa zikiandaliwa kwa mfumo wa asilimia arobaini (40%) na mtihani wa mwisho asilimia sitini (60%). Pamoja na kwamba Baraza halijawahi kuutumia mifumo hii tangu ilipowekwa, kumekuwa na mitazamo, maoni na mapendekezo tofauti katika muundo na matumizi ya alama za CA. Kuna mawazo pia kwamba mfumo wa CA kuchangia matokeo ya mwisho ya mwanafunzi pia utumike kwa watahiniwa wa kujitegemea (private candidates). Kwa sasa matokeo ya mitihani ya watahiniwa hawa yamekuwa yakitumia alama za mtihani wa mwisho tu na hivyo kutafsiriwa kama utaratibu ambao unamwonea mwanafunzi ambaye anahamu ya kujiendeleza kielimu lakini anakwama kwa sababu mfumo unaotumika siyo rafiki kwa mtahiniwa.
 
Kwa mantiki hii, Wizara imedhamiria kufanya harmonization ya masuala ya alama katika mitihani ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita ili kupata muundo mmoja na ulio wazi kwa wadau wote wa elimu ya sekondari. Lakini pia serikali imedhamiria kuhakikisha tathmini za wanafunzi katika ngazi mbalimbali zinakwenda sambamba na matarajio ya mitaala inayotumika na ambayo inahuishwa mara kwa mara ili iendane na wakati na mahitaji ya elimu katika ngazi mbalimbali.
 
VIWANGO NA UTARATIBU KUANZIA MWAKA 2013 KWA KIDATO CHA NNE NA MWAKA 2014 KIDATO CHA SITA 
Baada ya kufanya tathmini ya maoni mbalimbali ya wadau, misingi ifuatayo ilizingatiwa katika maamuzi kuhusu makundi ya alama na muachano wake:
 
a) Alama zitakazotumika zitakuwa A, B, C, D, E na F. Muachano wa alama kati ya kundi moja hadi jingine utafanana, isipokuwa tu pale ambapo itaonekana kuna sababu na hakuna athari za kuwa na muachano tofauti na ule ambao umetumika katika makundi mengine.
 
b) Makundi ya alama hayatakuwa na clusters isipokuwa pale ambapo itaonekana kufanya hivyo kunaleta tija katika kupata picha ya wahitimu kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Kwa mantiki hii
 
(i) makundi ya alama A, C, D, E na F yabaki na cluster moja moja bali kundi la alama B litakuwa na clusters mbili. Kundi la kwanza litakuwa la wale ambao wamepata alama kati ya 50 mpaka 59 na litaitwa B na lingine litakuwa la wale ambao wamevuka uwigo wa 50 hadi 59 na kuelekea uwigo wa 60 hadi 74 na hili litaitwa B+ (angalia jedwali hapo chini).
 
(ii) Pamoja na kuwa na muachano wa alama 26 kama jedwali linavyoonesha hapo chini, alama A kwa miaka mingi imekuwa ikianzia alama 75 hadi 100 na kwamba pamoja na uwigo huo bado wanaofaulu kwa kiwango hicho ni wachache sana. Kwa mantiki hii, hakuna haja ya kubadilisha uwigo ila juhudi ziendelee katika ufundishaji na ujifunzaji ili kiwango cha ufaulu kiongezeke na kupata wanafunzi wengi zaidi wanaofaulu katika kundi hili.
 
(iii) Pia, pamoja na kuwa na muachano wa alama 20 kama jedwali linavyoonesha hapo chini kwa miaka mingi, huko shuleni mwanafunzi aliyepata alama 21 na hadi 30 alihesabiwa kuwa na ufaulu wa chini kabisa au hafifu kwa kiwango cha alama D na ingawa ilikubalika ufaulu wa aina hiyo kwa mazingira ya nchi yetu unaridhisha. Alama F ilikuwa ni kwa wale waliopata chini ya hapo. Hivyo, alama F itaendelea kuwepo na itaanzia alama 0 hadi 19 na E itaanzia alama 20 hadi 29 na D – 30 -39. Lengo la muundo huu ni kuwa alama mbalimbali, isipokuwa kwa makundi machache, zianzie kwenye 0 yaani 0, 10, 20, 30, 40 na kuendelea badala ya kuanzia kwenye moja yaani 1, 11, 21, 31, 41 na kuendelea. Hii ni kwa ajili ya kuleta mtizamo unaofanana katika ngazi mbalimbali za elimu ambapo kwa sasa ngazi ambazo siyo za elimu msingi na sekondari zinatumia muundo wa kuanzia kwenye 0 badala ya 1.
 
c) Uwigo wa jumla wa alama kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita utaendelea kuwa wa alama 0 hadi 100 na kila kundi katika uwigo huu limepewa tafsiri kwa ajili ya kuamua mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya mwanafunzi kulingana na malengo ya mtihani husika. Kimsingi, tafsiri zifuatazo zitakatumika
 
(i) Alama A itakuwa na maana ya ufaulu uliojipambanua (distincion or outstanding performance),
 
(ii) Alama B+ itakuwa na maana ya ufaulu bora sana (excellent performance),
 
(iii) Alama B itakuwa na maana ya ufaulu mzuri sana ( very good perfomance),
 
(iv) Alama C itakuwa na maana ya ufaulu mzuri (good performance);
 
(v) Alama D itakuwa na maana ya ufaulu wa wastani (low performance),
 
(vi) Alama E itakuwa na maana ya ufaulu hafifu (very low performance), na
 
(vii) Alama F itakuwa na maana ya ufaulu usioridhisha (unsatisfactory performance).
 
Wataalamu katika maeneo mbalimbali ya elimu na ulimwengu wa kazi, kwa kushirikiana na Wizara, watatoa maana ya tafsiri hizi kiutendaji katika maeneo yao kulingana pia na mahitaji yao.
 
d) Alama C iwe ndiyo alama ya ufaulu mzuri ambao hauhitaji urekebu wa lazima, wakati alama D na E ni alama za ufaulu unaohitaji urekebu kadri mwanafunzi atakavyokuwa anaendelea na masomo ili kuthibitisha kama mlengwa anaweza na kulingana na mahitaji ya eneo husika (targeted remediation). Alama F iwe alama ya eneo linalohitaji urekebu wa hali ya juu (intesive remediation) ili mwanafunzi huyo aweze kumudu masomo kadri anavyoendelea kukua kielimu ama atakapoingia katika ulimwengu wa kazi.
 
e) Makundi ya alama yatajumuisha CA kwa kiwango cha asilimia isiyozidi 40 na mtihani wa mwisho kwa asilimia isiyozidi 60 kwa makundi yote ya watahiniwa ikiwemo wale wa kujitegemea (private candidates). Hii ni kwa kuzingatia kwamba CA siyo vizuri izidi uwigo wa alama ya ufaulu mzuri unapoanzia ambayo ni C au 40.
 
f) CA kwa upande wa Kidato cha Nne zitokane na mtihani wa Kidato cha Pili (alama 15), matokeo ya Kidato cha Tatu (alama 5 kwa kila muhula, na hivyo jumla ya alama 10), mtihani wa Mock (alama 10) na kazi mradi au Projects (alama 5). Kwa upande wa Kidato cha Sita, CA iendelee kutokana na muundo unaotumika sasa.
 
g) CA zitumike pia kwa watahiniwa wa kujitegemea. Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegmea ambao wanarudia Mitihani, CA zao zitumike zile zilizotumika kutoa matokeo yake ya mitihani ya awali. Kwa watahiniwa wa kujitegemea waliopitia mfumo wa Qualifying Test (QT), matokeo ya QT yatumike kama CA na mtihani wa mwisho uchangie alama 60.
 
h) Kwa vile alama endelevu kwa mwaka 2013 kwa wanafunzi wa Kidato cha Nne tayari zimeshawasilishwa Baraza la Mitihani Tanzania, alama hizo zichangie asilimia 40 katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2013.
 
i) Muundo wa wastani wa alama katika ufaulu (Grade Points Average ama GPA) utaandaliwa na kuanza kutumika pale utakapokuwa tayari na wadau wataelimishwa kuhusu muundo huo ili wapate kuufahamu na manufaa yake katika elimu ya sekondari.
 
j) Muundo huu mpya wa alama utatumika kwa mzunguko wa miaka minne kabla haujahuishwa tena ili kuupa muda wa kutosha kuona aina ya changamoto zinazojitokeza na jinsi ya kuzishughulikia. Aina hii ya muda itaruhusu vidato vinne vya elimu ya sekondari ya kawaida na nane ya elimu ya sekondari ya juu kupimwa. Hata hivyo, uhusihaji wa masuala ya mitihani unaweza ukafanyika iwapo matokeo ya uhuishaji wa mitaala kwa ujumla utahitaji pia eneo la mitihani liguswe na kuhuishwa pia.
 
Kwa mantiki hii, viwango vya alama na ufaulu ni kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 1 hapa chini:
 Jedwali Na 1
 MUUNDO WA ALAMA NA UFAULU

ALAMA
UWIGO WA ALAMA
IDADI YA ALAMA
TAFSIRI
A
75 - 100
26
Ufauli Uliojipambanua
B+
60 - 74
15
Ufaulu bora sana
B
50- 59
10
Ufaulu mzuri sana
C
40 - 49
10
Ufaulu mzuri
D
30 - 39
10
Ufaulu Hafifu
E
20 - 29
10
Ufaulu hafifu sana
F
                     0 - 19
20
Ufaulu usioridhisha

Kwa aina hii ya muundo wa alama, na kwa kuwa muundo wa GPA utaanza kuandaliwa na wadau kuelimishwa kabla haujaanza kutumika, katika kipindi hiki mpaka wakati huo, muundo wa madaraja utakuwa kama inavyooneshwa kwenye jedwali la 2 hapa chini.
 Jedwali Na 2
 MUUNDO WA MADARAJA

MUUNDO WA ZAMANI
MUUNDO MPYA
MAELEZO
POINTI
DARAJA
POINTI
DARAJA

7-17 17-17IKundi la ufaulu uliojipambanua na bora sana
18-21II18-24IIKundi la ufaulu mzuri sana
22-25III25-31IIIKundi la ufaulu mzuri na wa wastani
26-33IV32-47IVKundi ufaulu hafifu
34-35048-49VKundi la ufaulu usioridhisha
Wataalamu wa mifumo ya mitihani watalifanyia kazi zaidi jedwali hili la madaraja ili liweze kutumika kwa ufanisi katika kipindi hiki cha mpito. 
Kwa mantiki hii, Daraja Sifuri linafutwa na kuwekwa daraja litakalojulikana kama Daraja la Tano na ambalo litakuwa ndilo la mwisho kabisa katika ufaulu.
 
HITIMISHO 
Mabadiliko haya yamefanyika ili kuendelea kuimarisha mfumo wetu wa elimu na kuweka wazi taratibu mbalimbali kwa ajili ya mitihani na masuala mengine. Yako mambo mengi mengine ambayo hayana budi kuendelea kuimarishwa ikiwemo mfumo wa mitaala, walimu, mazingira ya kujifunzia na kufundishia pamoja na vitabu na vifaa vingine muhimu katika elimu. Masuala haya yanaendelea kuangaliwa kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ama Big Results Now (BRN). Ushirikiano wa wadau wote ili kuleta tija kwenye elimu ni muhimu sana na hivyo wizara itaendelea kuwashirikisha wadau wote kwa kadri itakavyohitajika na wadau pia wanaombwa wasiache kuishirikisha wizara pale watakapokuwa na jambo lolote ambalo linahitaji ushirikiano ili kwa pamoja tuweze kupata mafanikio katika sekta ya elimu.
Imetolewa, 
KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

NUSU UTUPU YA LINAH YACHANGANYA MIDUME


Linah akiwa jukwaani wakati wa shoo ya Fiesta 2013 jijini Dar.

Mavazi ya nusu utupu ambayo msanii Esterlina Sanga ‘Linah’ hupenda kuyavaa hasa kwenye matamasha yamekuwa yakiwadatisha wanaume na wengine kuomba kupiga naye picha kwa lengo la ‘kujipoza’ kama ilivyotokea kwenye Fiesta, Dar hivi karibuni.
  


Linah akipozi na baadhi ya wanaume walioomba kupiga naye picha.
  
Ijumaa limekuwa likimfuatilia Linah na kubaini kuwa kila mara hupenda kuvaa nguo zinazoacha wazi mapaja na kitovu chake na watu ambao amekuwa akipiga nao picha ni wanaume ambao wengi huonekana wakiwa wamemshika kimahaba.

Hata hivyo, licha ya mwenyewe mara kadhaa kueleza kuwa, hayo ni mvazi ya kikazi zaidi, baadhi ya mashabiki wamemponda na kumtaka kubadilika hasa ikifahamika kuwa ni mtoto aliyetokea kwenye familia iliyoshika dini na kwamba kuvaa hivyo ni kujidhalilisha.

GPL

PICHA ZINATISHA: ANAYEDAIWA KINARA WIZI WA ‘POWER WINDOW’ AKAMATWA,APEWA KICHAPO NUSURA AFE

Link Mbaga baada ya kula kichapo cha nguvu kutoka kwa wananchi wenye hasira kali

MKAZI mmoja wa Sinza Lion jijini Dar, Link Mbaga (25) Jumanne iliyopita alinaswa maeneo ya Sinza Afrikasana na kuchezea kichapo kutoka kwa watu wenye hasira akidaiwa kutaka kuiba vifaa vya kwenye gari aina ya Toyota Harrier, Ijumaa limeinyaka. 
Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, alisema Mbaga na wenzake wanne wanaodaiwa kuwa ni vinara wanaounda mtandao wa kuiba power window kwenye magari walifika eneo la tukio wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Noah.
Mbaga akisulubiwa na wananchi.
“Lengo lao lilikuwa ni kuiba kwenye gari la mteja wa Hospitali ya Marie Stop lililokuwa limeegeshwa nje ya hospitali hiyo,” alisema shuhuda huyo.
Gari aina ya Toyota Harrier walilotaka kuiba power window Mbaga na wenzake.
Shuhuda huyo alisema Mbaga na wenzake walifanikiwa kulitoboa gari hilo na kuchukua simu mbili pamoja na kompyuta mpakato ‘laptop’.
“Kabla ya kumalizia zoezi lao mlinzi wa hospitali hiyo aitwaye Jonas Mwakajinga aliwasikia ndipo alipofika na kuwakurupusha,” kimesema chanzo hicho.
Wananchi wakiwa wameandaa tairi tayari kumtia kiberiti Mbaga kabla ya polisi kufika eneo la tukio na kumnusuru.
Inadaiwa watuhumiwa wengine walifanikiwa kutoroka kwa kutumia gari walilofika nalo lakini mlinzi aliwahi kumng’ang’ania Mbaga na kuanguka naye chini.
Wakati mlinzi akipambana na Mbaga wananchi wenye hasira walifika eneo la tukio na walipopata maelezo walianza kumpa kichapo cha kufa mtu mtuhumiwa huyo wakisema itakuwa fundisho kwa wengine.
Kipondo kikiwa kimepamba moto kwa Mbaga.
Wakati akipewa kichapo hicho, Mbaga alijitetea kwamba hakuwa mwizi bali ni mfanyakazi wa kampuni moja ya simu.
“Mimi kazi yangu ni data manager niko maeneo ya Mlimani City, naishi Sinza Lion kwa Massawe,” alisema kijana huyo.


Mbaga akiwa hoi baada ya kichapo.
Mbali na kusema hivyo, Mbaga alidai kwamba ameoa na mkewe anaitwa Fausani na kabla ya kufika hapo alikuwa na rafiki yake wakinywa pombe Mlimani City.
Wananchi wakishuhudia tukio hilo.
“Nilikuwa nakunywa Pombe na Leonard pale Mlimani City, jamani naomba mnionee huruma, wale jamaa walinipa lifti tu,walikuwa wako wanne ila nawafahamu,” alisema Mbaga.

Polisi wakijaribu kuchukua maelezo ya mtuhumiwa baada ya kuwasili eneo la tukio. 

Polisi wakimbeba Mbaga kumpeleka kwenye difenda.
Mbaga aliokolewa na askari waliotokea na kumbeba msobemsobe hadi katika Kituo cha Polisi cha Mwananyamala.
Kutokana na hali mbaya ya mtuhumiwa huyo, askari hao walilazimika kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala ili aweze kupata matibabu.

Mbaga akiingizwa kwenye difenda. 

Safari ya kuelekea Mwananyamala ikaanza.