aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, November 1, 2013

WABUNGE NA MISHAHARA YAO....JE NI HALALI KWAO KULALAMIKA MASLAHI MADOGO?!



Imethibitika rasmi kuwa wakati wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wakilalamikia maslahi madogo, mbunge mmoja hulipwa mshahara wa Sh. milioni 11 kwa mwezi.

Kiasi hiki hakijumuishi posho ya Sh. 330,000 anayolipwa mbunge kwa kuhudhuria kikao kimoja kwa siku. Posho ni Sh. 80,000 za kujikimu akiwa nje ya jimbo lake, posho ya vikao Sh. 200,000 kwa siku na mafuta ya gari Sh. 50,000, jumla kuwa Sh. 330,000 kwa siku.

Aidha, mbunge mmoja hulipwa ‘gratuity’ (kiinua mgongo au bahashishi) ya Sh. milioni 72 baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka mitano cha ubunge.

Aidha, wabunge hupewa fedha za Mfuko wa Jimbo Sh. milioni 30 kila mwaka kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo katika majimbo yao.

PICHA:HABARI KAMILI KUHUSU KIFO CHA MTOTO WA MIAKA 4,JOSHUA ISACK ALIYEFIA NDANI YA SHIMO LA CHOO CHA JIRANI MBEYA.

Mwili wa Mtoto Joshua Isack (4) ukichukuliwa na polisi
Hili ndilo shimo alimokutwa  marehemu Joshua

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Mtoto Joshua Isack (4) aliyepotea nyumbani kwao akiwa anacheza na watoto wenzie kwa siku tatu akutwa akiwa amefariki dunia ndani ya shimo la choo cha jirani na kuzua maswali ya sintofahamu kwa wazazi na majirani.
Tukio hilo la kuonekana kwa mtoto huyo lilitokea jana majira ya saa Kumi jioni katika Mtaa wa Nyibuko Pambogo kata ya Iyela Jijini Mbeya baada ya juhudi za wazazi na majirani kushirikiana kumtafuta na kumpata akiwa amepoteza maisha ndani ya shimo la choo.
Akizungumza kwa uchungu na masikitiko makubwa baba mzazi wa marehemu Isack Daniel ambaye ni mfanyakazi wa Mamlaka ya Maji Mbeya alisema Mtoto wake huyo wa kiume alikuwa anacheza na wenzie jumatatu ya Oktoba 28,  majira ya saa 12 jioni lakini alitoweka katika mazingira ya kutatanisha.
Alisema baada ya kuona giza linaingia na mtoto hajarudi alianza kumtafuta katika kila eneo akishirikiana na baadhi ya ndugu na majirani lakini hakufanikiwa kumwona kwa siku hiyo ambayo kesho yake akiwa ni viongozi wa mtaa walienda kutoa taarifa kituo cha Polisi cha Kati Mbeya Mjini.
Mzazi huyo aliendelea kusema baada ya kutoa taarifa polisi bado waliendelea na juhudi za kumtafuta huku Ubalozi ukiunda kikosi maalumu cha kufanya msako wa nyumba hadi nyumba ambapo baada ya kupita katika nyumba ya jirani alipokutwa marehemu katika shimo la maji machafu walipatwa na wasi wasi baada ya kuona kuna mabadiliko ya mbao zilizokuwa zimefunika shimo hilo.
Alisema awali walivyopita siku moja kabla waliona shimo hilo likiwa limefunikwa kwa mabanzi yaliyochakaa lakini siku ya pili yake asubuhi walikuta kukiwa na mabanzi mapya kuashiria kuna ukarabati umefanyika hali iliyowapa wasi wasi na kulazimika kulifunua shimo hilo na kumkuta marehemu akiwa amepoteza maisha ndani ya shimo  hilo.
Alisema aliyegundua kuwepo kwa mtoto ndani ya shimo ni ndugu yake alikuwa katika msako wa nyumba kwa nyumba na ndipo alipompigia simu akiwa kazini nayeye kutoa taarifa polisi na kwenye Serikali ya Mtaa ambapo walianza kufanya juhudi za kumtoa lakini walikwama hali iliyowalazimu kuomba msaada kwa kikosi cha Zimamoto na Uokoaji waliofanikiwa kumtoa majira ya saa Kumi jioni.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Nyibuko Pambogo kata ya Iyela Mage Makwenda alisema akiwa ofisini kwake alipokea taarifa za kupotea kwa mtoto katika mazingira ya kutatanisha lakini wakiwa katika juhudi za kumtafuta ndipo walioteuliwa kufanya upelelezi na msako mkali walipotoa taarifan za kuonekana kwa mtoto akiwa amefariki dunia ndani ya shimo la maji machafu.
Alimtaja mmiliki wa nyumba hiyo kuwa ni Gesho Kibonde (43) mkazi wa Mtaa wa Nyibuko kata ya Iyela Jijini hapa ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano pamoja na mkewe.
Kwa upande wake majirani na wakazi wa mtaa huo ambao hawakutaka majina yao kuandikwa walisema tukio hilo lina utata mkubwa kwa sababu baada ya mtoto kuonekana ndani ya shimo baadhi yao walifanikiwa kuchungulia na kumkuta marehemu akiwa amesimamishwa mithiri ya kutumbukiwa na mtu.
Mashuhuda hao waliendelea kusema kama mtotio angekuwa ametumbukia kwa bahati mbaya akiwa anacheza na wenzie angeonekana kuumia baadhi ya viungo lakini haikuwa hivyo pamoja na kuonekana kufa maji machafu ndani ya shimo hilo basi tumbo lake lingejaa lakini hali aliyokutwa nayo marehemu ni tofauti.
Hata hivyo wengine wamelihusisha tukio hilo na imani za kishirikina kwa madai kuwa aliyewaonesha kuwepo kwa mtoto ndani ya shimo hilo ni babu kutoka Mwakaleli( mganga)ambaye alifuatwa na baadhi ya watu ili kusudi awaoneshe mtoto na ndipo babu huyo alipo waambioa warudi katika nyumba ya jirani watamkuta akiwa hai.
Walisema baada ya kurudi na kutafuta katika eneo hilo waliokuta akiwa amekufa kitu ambacho waliamini ni kuchelewa kufika na kuligundua eneo lakini wanrwahi huenda wangemkuta marehemu akiwa mzima kabisa.

Aidha wakati zoezi la kumtoa marehemu ndani ya shimo hilo kwa ushirikiano wa Jeshi la Polisi, Zimamoto na Uokoaji pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Mbeya( Mbeya uwsa) vilio vilitawala eneo hilo kutoka kwa wanawake walioshindwa kujizuia huku wengine wakipoteza fahamu na kulazimika kupewa msaada

UONEVU!! MSICHANA ABAKWA NA KUNDI LA WANAUME NA KUTUPWA KWENYE SHIMO LA CHOO,WATUHUMIWA WAPEWA ADHABU YA KUKATA NYASI NA KUACHIWA HURU..


MAMIA ya waandamanaji nchini Kenya wamewasilisha polisi hati ya kutaka kukamatwa kwa watuhumiwa waliombaka msichana huyo wa miaka 16.
Msichana huyo alibakwa na kundi la wanaume na kutupwa katika shimo la choo ambapo alivunjika mgongo wake.
Wanaume wanaotuhumiwa kumbaka msichana huyo waliamriwa na polisi kukata nyasi kama adhabu ya kitendo hicho.

Hati hiyo ya kutaka kuwafungulia mashitaka watuhumiwa wa ubakaji imetiwa saini na watu milioni 1.2 wakitaka watuhumiwa kukamatwa haraka na kuwafikisha mahakamani.
Waandamanaji hao wameelezea kukasirishwa na adhabu hiyo na kuhoji kwa nini polisi hawakufanya uchunguzi ili kumtendea haki msichana huyo.
Pia wanataka polisi waliowaadhibu washukiwa na kisha kuwaachilia, wakamatwe na kufunguliwa mashitaka.

Tayari wanawake milioni 1.2 wameunga mkono kampeini hiyo iliyoanzishwa na mwanaharakati Nebila katika mtandao wa kijamii wa Avaaz ulio na wanachama milioni ishirini na saba kote duniani na inaarifiwa idadi ya wanawake wanaopinga kitendo cha wabakaji na kile cha polisi kuwaadhibu kwa kukata nyasi, inaendelea kuongezeka.

Kampeini hii imekuja baada ya msichana Liz kubakwa na genge la wanaume sita ambao baadaye walimtupa ndani ya shimo la choo.
Liz alipata majeraha mabaya sana na hata kuvunjika uti wa mongo na sasa amelazimika kutumia kiti cha magurudumu na hadi sasa amefanyiwa upasuaji katika sehemu zake za siri.
Polisi waliwakamata watuhumiwa watatu kati ya sita waliodaiwa kumbaka msichana huyo, lakini baadaye wakawaachilia baada ya kuwaadhibu kwa kukata nyasi nje ya kituo cha polisi. BBC

VIDEO: MDOGO WAKE DIAMOND ATOA VIDEO YA KUONYESHA MAISHA YA DIAMOND KABLA HAJATOKA



AFUNGWA MIAKA 30 NA KUCHAPWA VIBOKO 12 KWA WIZI WA PIKIPIKI.



MKAZI wa Makongorosi, wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Januari Juma (30), amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko12 baada ya kupatikana na kosa la ujambazi wa kutumia silaha.
Adhabu hiyo iliyotolewa baada ya Juma kukiri mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, kutenda kosa la kupora pikipiki, simu ya mkononi na fedha taslimu sh 45,000.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka, Thomas Kilakoi, kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 6 mwaka huu, akiwa na wenzake wanne, Frank Peter, George Lwanji, Hussein Feli na Ericko Sikujua.
Alidai kuwa kwa pamoja washtakiwa walimvizia njiani Aggrey Mwezimpya mkazi wa kijiji cha Mkusi na kumpora vitu hivyo baada ya kumtishia kumkata kwa mapanga.
Mbele ya Hakimu Adamu Mwanjokolo, Kilokoi aliendelea kudai kuwa baada ya kumpora Mwezimpya vitu hivyo saa moja jioni, watuhumiwa waliondoka na kukimbilia katika kijiji cha Mwaoga wilayani Chunya ambako walikamatwa na polisi wakiwa na pikipiki hiyo.
Mara baada ya kusomewa mashtaka hayo, Juma alikiri kutenda kosa hilo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 huku wenzake wanne wakikana mashtaka na kurejeshwa mahabusu hadi kesi yao itakapotajwa tena.
Mwandishi ni Sammy Kisika, Sumbawanga

MAGAZETI YA BONGO LEO 1/11/2013..


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

UFOO SARO ALA KIAPO CHA SIRI BAADA YA KURUHUSIWA HOSPITALINI...

Ufoo Saro akiwa hospitali baada ya kupigwa risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther Mushi.

SIKU chache baada ya Mtangazaji wa Runinga ya ITV, Ufoo Saro kuruhusiwa hospitalini alipokuwa amelazwa baada ya kudaiwa kupigwa risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther Mushi, ameibuka na kula kiapo cha siri. 
Ufoo ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, katika tukio la yeye kupigwa risasi, alimpoteza mama yake mzazi aitwaye Anastazia Saro aliyedaiwa kuuawa na marehemu Mushi aliyejiua kwa risasi.
Akizungumza na gazeti hili Ufoo alisema, kamwe hawezi kusema kilichokuwa kikiwagombanisha yeye na marehemu Mushi mpaka siku ya mwisho wa uhai wake.
Ufoo Saro.
“Siwezi kuzungumzia kabisa chanzo wala ugomvi wetu mimi na marehemu Mushi. Hiyo itakuwa siri yangu,” alisema Ufoo.
Katika mahojiano na gazeti hili, mtangazaji huyo alipoulizwa kuhusu msimamo wake wa uhusiano baada ya kupona kabisa alisema, hawezi kujiingiza tena kwenye mapenzi kwa sasa.
“Sitaki kabisa kusikia juu ya mapenzi, siwezi kuliweka suala hilo akilini tena,” alijibu kwa kifupi kwa sauti ya chini lakini yenye mkazo.