![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdW1vgDRRPg5hS-IDQvf_mXYV1POwdNV6O5vG_uLQPf4zzG4XTHesZXqxsrKPRzmShvIuq6J3UGAtanyVh9mnA_Lg4J8wXm1469mWcK8XVKuw353QRELXplu3EBvxmdXEgmr-GOz-a6b4/s1600/1.jpg)
Wanawake wanne wa Kitanzania wamekamatwa katika jimbo linalojitegemea la Macau, nchini china wakituhumiwa kufanya biashara ya ukahaba na wengine kwa kusafirisha watu kwa lengo la kufanya biashara ya ngono. kinyume cha sheria (human trafficking)....
Polisi walipewa fununu kuwa kuna biashara ya ukahaba inafanyika katika hoteli moja iliyopo jimboni humo. Polisi walipofanya msako, walikuta wanaume wawili na wanawake 38, wote Watanzania, katika vyumba vitano vya hoteli hiyo...
Mmoja wa wasichana hao amewaambia polisi wa Macau kuwa aliendaChina baada ya kuahidiwa nafasi ya kazi na mwanamke mwingine aliyekutana naye Tanzania, lakini alipofika huko, akalazimishwa kufanya ukahaba...
Aliwaambia polisi hao kuwa amekua akikataa kufanya ukahaba na kutaka kurudi Tanzania lakini wenyeji wake wamekuwa wakimpiga na kumlazimisha kuuza mwili...
Jimbo la Macau taratibu linaongezeka kuwa maarufu kwa Watanzania kukamatwa kwa tuhuma za biashara haramu.
Nadhani wengi mnakumbuka ni jimbo hili hili ambapo mrembo maarufu nchini, Jackie Cliff alikamatwa kwa tuhuma za kusafirisha madawa ya kulevya.
Nadhani wengi mnakumbuka ni jimbo hili hili ambapo mrembo maarufu nchini, Jackie Cliff alikamatwa kwa tuhuma za kusafirisha madawa ya kulevya.
Angalia video hapo chini:
No comments:
Post a Comment