MTOTO wa kike mwenye umri wa miaka mitatu, Maryment Ibrahim ambaye anaishi Tandale jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alipatwa na masahibu makubwa baada ya kutekwa nyara na kutoroshwa hadi Gairo mkoani Morogoro huku mtekaji akidaiwa kutaka apewe shilingi milioni 6 ili amuachie.
Awali, ilidaiwa Ramadhan alikuwa na tabia ya kuwachukua watoto wadogo wa mtaani hapo na kuondoka nao na kuwarudisha baadaye, kitu kilichowafanya wazazi wa mtoto huyo kutokuwa na wasiwasi.
Mtuhumiwa wa utekaji.
Wakizungumza na mwandishi wetu, wazazi wa mtoto huyo walisema waliamua kutoa taarifa polisi na kufunguliwa jalada nambari KJM/RB/8994/13 baada ya kupashwa kuwa mtekaji ambaye alishaacha kazi yake ya kukaanga chipsi, aliondoka muda mrefu na binti yao na hakukuwa na dalili za kurejea.Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu, wazazi hao pamoja na majirani walifanya uchunguzi wa chinichini na kufanikiwa kupata namba ya simu ya mtekaji huyo, lakini walifanikiwa kubadilishana naye ujumbe mfupi wa simu kwani hakuwa akipokea simu yake ya kiganjani.
Mtoto Maryment Ibrahim aliyetekwa na Ramadhan.
Wazazi hao walisema kuwa Oktoba 19 mwaka huu mmoja wa majirani walioguswa na tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Justin Henry alijitolea kusafiri mpaka Gairo kumsaka mtoto na mtekaji wake jambo ambalo lilifanikiwa kwa kumpata mtoto akiwa mzima wa afya japokuwa mtekaji alishtukia na kukimbia.
No comments:
Post a Comment