Barcelona imesema kwamba mshambuliaji wake mpya kutoka Brazil
Neymar ameanza kuugua ugonjwa wa upungufu wa chembe hai
nyekundu za damu (Anaemia), lakini ugonjwa huo hautomfanya
asiendelee na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya.
Timu ya madaktari wa mabingwa wa La Liga wamesema kwamba
waligundua mpangilio usiofaa wa damu ambao unaathiri uzalishaji
wa chembe hai nyekundu za damu wakati mshambuliaji huyo
alipofanyiwa vipimo vya damu.
Neymar, ambaye alijiunga na Barcelona kwa ada ya uhamisho
inayozidi £50million, ameanza matibabu maalum.
Barcelona imeaambia Associated Press kwamba kutokana na
upasuaji aliofanyiwa wiki kadhaa zilizopita wa tonsils
umesababisha aanze kuugua Anaemia lakini tayari ameanza
matibabu na jambo hilo halitomzuia kuendelea na mazoezi na
wachezaji wenzake.
No comments:
Post a Comment