marriage-1
KATIKA Hali ya isiyo kuwa ya kawaida, Bilionea wa Hong Kong ametangaza dau la zaidi ya Paundi 40 milioni kwa mwanaume yeyote anayeweza kumuoa binti yake msagaji.
Mfanyabiashara huyo wa meli za biashara na mizigo na muendelezaji majengo Cecil Chao Sze –Tsung anaonekana kuchoshwa na mahusiano ya binti yake Kiki kwa binti mwingine wa kike kwa karibu miaka tisa.
Mfanyabiashara huyo wa Hong kong alikuwa na nia ya kumrithisha himaya yake binti yake huyo lakini kwa masharti ya kuolewa katika desturi za kistaarabu na siyo kuwa na mahusiano na mwanamke mwenzake.
Taarifa zinasema kwamba kwa kuangalia ukubwa biashara yake na amewapa baadhi ya makampuni zake wanawe wengine wawili na fedha za kutosha, lakini tajiri huyo Chao anataka wanawe wawe na maadili mema katika jamii na sitabia za ovyo.
Chao mwenye umri wa miaka 77 aliliambia gazeti la Malaysia Nanyang Siang Pau kwamba angeweza kutoa fedha mara mbili ya hizo katika kuvutia wanaume wengi kujitokeza kwa ajili ya kumuoa mwanae.
Binti huyo anaonekana kama amechanganyikiwa kwa uamuzi wa baba yake kumpa masharti ya kuolewa kabla ya kurithi mali na fedha taslimu za baba yake.
Amesema kwamba fedha si kitu cha kumvutia mwanaume au yeye kumpenda mwanaume kwa sababu ya kupenda ni utashi wa mtu binafsi.
“Napenda kuwa na furaha kufanya urafiki na mtu yeyote tayari kuchangia kiasi kikubwa cha fedha kwa jamii na upendo wangu ni kwa watu wote na si kwa sababu ya fedha za baba yangu,” amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya maendeleo ya Cheuk Nang, ambaye pia ni mwanaharakati wa LGBT anasema kwamba kwa kipindi kirefu watu wamekuwa wakikiuka haki za mashoga na ndiyo sababu ya kushirikiana karibu na Big Love Alliance ambacho ni kikundi cha kutetea haki za mashoga Hong Kong na kutaka haki za mashoga kuwa sheria na kupitishwa na serikali.

CHANZO-MOBLOG