aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 8, 2013

WAKATWAKATWA MAPANGA KWENYE UGOMVI KATI YA KOO MBILI...


WATU watatu wakazi wa kijiji cha Kewanja, Nyamongo wamelazwa katika Hospitali ya Sungusungu Nyamongo wakiwa katika hali mbaya, baada ya kukatwakatwa mapanga wakati wa ugomvi kati ya koo za Wanyabasi na Wanyamongo.
Ugomvi huo unatajwa kutokea katika mnada wa ng’ombe ambapo inadaiwa Wanyamongo walikuwa wakiwazuia Wanyabasi kwenda Mnadani katika Kijiji cha Kewanja na kusababisha mapigano kati ya koo hizo mbili.
Kamanda wa Polisi Tarime na Rorya, Kamishina Msaidizi Justus Kamugisha, alisema hivi karibuni kuwa mapigano hayo yalianza saa tatu asubuhi Agosti 5 mwaka huu, wakati vijana zaidi ya 200 jamii ya koo ya Wanyamongo, waliokuwa na silaha za jadi, walipojaribu kuwazuia Wanyabasi kwenda mnadani kuuza ama kununua mifugo.
Kamanda Kamugisha aliwataja waliojeruhiwa ambao kwa sasa wamelazwa katika Hospitali ya Sungusungu Nyamongo, wakiwa katika hali mbaya kutokana na majeraha, kuwa ni mkazi wa kijiji cha Nyakunguru Matiko Moagi (20), mkazi wa kijiji cha Kewanja, Masaba Kihinda (20) na mkazi wa kijiji cha Kewanja, Mwita Itembe (21).
Wakati wa mapigano hayo mwanafunzi kidato cha nne, Shule ya Majimoto Wilaya ya Serengeti, Maxmilian Nyanchia (21), aliyekuwa akipita na pikipiki, alisimamishwa na kupigwa huku pikipiki aliyokuwa nayo aina ya SanLG yenye namba T 238 CCV, mali ya Michael Makori ikichomwa moto na kuteketea.
"Polisi kwa kushirikiana na raia wema inawasaka watuhumiwa waliohusika katika tukio hilo wakiwemo watu wanaochochea mapigano kati ya koo hizo mbili, ili wachukuliwe hatua za kisheria…hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusu tukio hilo,” alisema Kamanda Kamugisha

No comments:

Post a Comment