aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 8, 2013

WAFANYAKAZI ZANZIBAR KULIPWA MISHAHARA OFISINI...


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee, alisema hayo wakati alipozungumza na gazeti hili kuhusu kutafuta watumishi hewa, ambao wanadaiwa wapo katika baadhi za wizara za SMZ.
Alisema utaratibu wa kuhakiki na kulipa mishahara ya watumishi ofisini, umeanza kwa wafanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, pamoja na walimu wote wa shule za unguja na Pemba.
“Wizara ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, imesikiliza kilio cha wawakilishi na sasa tumeanza kuhakiki watumishi wote kwa kurudisha utaratibu wa zamani wa kupokea mishahara ofisini na sio katika benki,” alisema.
Akifafanua zaidi, Mzee alisema Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, imepewa kazi ya kuhakiki watumishi wote wa SMZ.
Alisema Serikali imesimamisha utaratibu wa watumishi wake waliokuwa wakipokea mishahara katika benki mbali mbali kwa muda, ili kutoa nafasi ya uhakiki.
Mzee alisema mara baada ya kukamilika kwa uhakiki wa watumishi hewa, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, atakagua watumishi wastaafu wanaopokea viinua mgongo ili kutafuta wastaafu halali.
Alisema juhudi hizo zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, lengo lake ni kufichua watendaji wanaojishughulisha na ubadhirifu wa mali za umma.
Kauli ya Mzee iliungwa mkono na Mwenyekiti wa Kuchunguza Hesabu za Mashirika ya Serikali (PAC), Omar Ali Shehe, wakati akiwasilisha maoni ya kamati hiyo.
Alisema uchunguzi umebainika kwamba mashirika ya umma na vikosi vya Serikali upo ubadhirifu mkubwa unaotokana na ukiukwaji wa taratibu za mahesabu.
Shehe aliitaka Serikali kufanya ukaguzi wa mishahara ya watumishi wa Serikali katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambako viko vikosi vya SMZ.
“Tunaitaka Serikali mara baada ya kumaliza kazi ya kuhakiki watumishi katika Wizara ya Elimu iendelee moja kwa moja katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,” alisema.
Mwishoni mwaka jana watumishi hewa kadhaa walibainika katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment