aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Monday, August 12, 2013

VIFO VYA SAMAKI VYAZUSHA HOFU TANZANIA,MALAWI...


VIFO vya samaki katika ziwa Nyasa katika Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, vimezusha hofu kati ya Tanzania na Malawi kutokana na kila upande kuhisi umetupa fataki ziwani humo. Hisia hizo zinatokana na pande mbili hizo kuwa kwenye mgogoro wa mpaka.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt.Teresa Huvisa, akizungumza na wananchi kandoni mwa Ziwa Nyasa wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani Ruvuma, alisema;“Nimepata taarifa kuwa samaki wanaokufa katika Ziwa Nyasa sasa wameleta hofu kwa wananchi wa nchi zote mbili Tanzania na Malawi, kwa hiyo ninachoweza kuwaambia ni kwamba tutatuma wataalamu kuchunguza chanzo cha samaki kufa,” alisema Dkt. Huvisa.
Lakini pia kuna wavuvi wanatumia majani yanayoitwa mtunungu kuvulia samaki ambayo ukimwaga ziwani au mtoni samaki wanakufa, kwa hiyo msitumie sumu kuvulia samaki.
Alisema samaki hao wanakufa ziwani humo bila kujua chanzo chake msiwale.
Hata hivyo aliwatoa hofu wananchi hao waishio mpakani mwa nchi ya Malawi na Msumbiji kutokana na mzozo wa kugombea umiliki na mpaka wa ziwa hilo kati ya Tanzania na Malawi, kutoogopa mzozo huo na kwamba Malawi haina ubavu wa kupigana na Tanzania endapo nchi hizo zitaingia vitani  

No comments:

Post a Comment