aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, August 9, 2013

Umeyasikia ya Winga Raheem Sterling.




image
Winga wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa 
ya England Raheem Sterlng amefikishwa 
mahakamani hii leo kujibu tuhuma za
 kumshambulia mtu baada ya kukamatwa usiku wa
 kuamkia leo (Alhamis).
Winga huyo mwenye umri wa miaka 18 alilala
 kwenye kituo cha Polisi eneo la 
Merseyside na alipanda kizimbani hii leo ambapo
 alikanusha kosa la kumshambulia mtu .
Sterling alikamatwa majira ya saa nne na nusu hapo
 jana ambayo kwa muda wa
 kitanzania ni saa sita na nusu baada ya polisi kuitwa 
eneo la Page Moss baada ya 
polisi kuitwa kufuatia vurugu zilizotokea
 kwenye eneo hilo .
image
Sterling alilazimika kulala ndani kwenye 
kituo hicho kabla ya kupandishwa 
mahakamani hii leo kujibu tuhuma hizo 
na amekewa dhamana yenye masharti 
ambapo shitaka lake litasikilizwa tena 
mwezi ujao (septemba 20).
Hii si mara ya kwanza kwa winga huyu 
mwenye vituko kuingia matatizoni na 
amewahi kupanda kizimbani mara moja 
kujibu shutuma kama hizo .
Raheem hivi majuzi aliitwa kwenye
 kikosi cha timu ya taifa ya England 
kwa vijana
 wenye umri chii ya miaka 21 kitakachovaana 
na Scotland wiki ijayo na bado kocha 
wa England Roy Hodgson hajatoa tamko lolote
 juu ya tukio hilo .

No comments:

Post a Comment