aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Friday, August 9, 2013

UKIMTONGOZA MSICHANA KWA KUTUMIA HAYA MANENO LAZIMA AKUBALI TU HAWEZI KATAA KWANI NI MTEGO HATARI SANAAA

Jamaa: Hello mrembo, samahani, una
mpenzi?
Binti: Hapana. Sina mpenzi.
Jamaa: Kitabu cha Mwanzo 2: 18 "Bwana
Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe
peke yake, nitamfanyia msaidizi wa
kufanana naye."
Binti: Lakini mimi sikupendi jamani.
Jamaa: Waraka wa kwanza wa Yohana 4:8
"Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa
maana Mungu ni upendo."
Binti: Mh! Mi ntajuaje kwamba na wewe
unamaanisha hayo maneno?
Jamaa: Injili ya Mathayo 12:34b "Maana,
kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo
wake."
Binti: Jamani leo kazi. Mi ntajuaje kwamba
we ni mkweli na mwaminifu?
Jamaa: Injili ya Marko 13:31 "Mbingu na
nchi zitapita; lakini maneno yangu
hayatapita kamwe."
Binti: Wewe! Na kwanini umekuja kwangu?
Wasichana mbona wako wengi tu!
Jamaa: Mithali 31:29 "Binti za watu wengi
wamefanya mema, Lakini wewe umewapita
wote."
Binti: We una mambo wewe! Sasa mimi
kwangu umependa kitu gani?
Jamaa: Wimbo Ulio Bora 4:7 "Mpenzi
wangu, u mzuri pia pia, Wala ndani yako
hamna ila."
Binti: Mh! Huo uongo, mbona mimi hata
sio mzuri kihivyo. Unaongeza chumvi tu!
Jamaa: Mithali 31:30 "Upendeleo
hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali
mwanamke amchaye Bwana, ndiye
atakayesifiwa."
Binti: Nikisema nimekukubalia itakuaje?
Jamaa: Mwanzo 2:24 " Kwa hiyo
mwanamume atamwacha baba yake na
mama yake naye ataambatana na mkewe,
nao watakuwa mwili mmoja."
Binti: Jamani we mkaka. Inakuaje unajua
maandiko kiasi hicho?
Jamaa: Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati
kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari
maneno yake mchana na usiku, upate
kuangalia kutenda sawasawa na maneno
yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo
utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo
utakapositawi sana."
Binti: Wowwww! Naona unampenda sana
Mungu.
Jamaa: Zaburi 34:8 "Onjeni mwone ya
kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule
anayemtumaini."
Binti: Mh! Haya bwana. Basi nipe muda
nifikirie ombi lako.
Jamaa: Wafilipi 4:8 "Hatimaye, ndugu
zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo
yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki,
yo yote yaliyo safi, yo yote yenye
kupendeza, yo yote yenye sifa njema;
ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri
yo yote, yatafakarini hayo."
Binti: Mh! Jamani wewe, haya, nimekubali.
Mpaka hapo nakupenda tayari!!
Jamaa: Ufunuo wa Yohana 22:21b "Amina"

No comments:

Post a Comment