aaaaa

Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 8, 2013

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA: NDUGU WAGOMA KUZIKA MAREHEMU WAKIAMINI MGANGA ATAMFUFUA NDUGU YAO



Dereva wa boda boda Cheni Abed akiwa chini baada ya pikipiki yake

 kugonga na baiskeli kwenye makutano ya barabara za Mafisa,Kichangani.
Dereva wa boda boda Aliyejulikana kwa jina Bw Cheni Abed kufariki dunia 

baada ya 
kugongana na baiskeli huku dereva wa baiskeli hiyo ambaye pia alimpakia mwanae 
wakiwa salama salmini.
Cheni ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Mchuma kata ya Kichangani mkoani 

hapo 
alipoteza maisha baada ya kugongana na baiskeli hiyo na kuangukia kichwa 
kwenye makutano ya barabara za Msamvu,Mafisa,Mwembesongo huku dereva 
wa baiskel hiyo ambaye alimpakia mwanae wakisalimika kwenye tukio hilo.

Umati wa watu ukishuhudi tukio hilo la aina yake

Kufuatia mazingira ya tukio hilo familia ya dereva boda boda huyo iliamua 

kusafiri hadi wilaya ya mvomero kwenda kwa mganga wa kienyeji kuchunguza 
mazingira ya kifo hicho ambapo Sangoma Hamis Masai mkazi wa kijiji cha 
Changarawe kata ya Mzumbe Wilaya ya Mvomero mkoani hapo alimueleza baba 
wa mzazi wa marehemu huyo Bw Abed Shabani kwamba mama yake mzazi ndiye 
alimuua mjukuu wake huyo kwa kumchukua msukule na kwamba Sangoma huyo 
alimhakikishia Mzee Shabani kwamba alikuwa na uwezo wa kumrejesha dunia 
mwanae huyo aliekuwa nguvu muhimu kwenye familia hiyo.


Kufutia kauli hiyo Mzee Shabani aliludi Morogoro mjini na kusitisha mazishi ya 

kijana wake kwa siku nne akisubiri mganga huyo amfufue, kufuatia taarifa hizo 
majirani ambao tayari walishaanza kutoa msaada wa kuchimba kaburi na kuchanga 
michango ya mtaa walizuiwa kufanya shughuri hizo kwa maelezo kwamba Cheni 
angefufuliwa.
Habari za kufufuka kwa boda boda huyo zilizagaa kwa kasi kubwa kama

 kile
 kimbunga cha sunami na kwamba siku ya nne aliyoahidi mganga huyo 
kumfufua boda boda huyo ilipofika umati wa watu kutoka kona zote za mji wa 
morogoro walifuka nyumbani kwa mzee Shabani akiwemo waandishi wa habari hizi 
kwa lengo la kushuhudia maajabu hayo. Na Dustan Shekidele..


Familia hiyo na wananchi hao walisubiri toka saa mbili asubuhi hadi 

saa moja usiku bila kushuhudi boda boda huyo akifufuliwa na kwamba 
Sangoma huyo alipoulizwa na familia hiyo alidai kwamba kuna mashariti 
yalivunjwa
 na familia hiyo hivyo asingeweza tena kumfufua marehemu wao na kwamba 
baada
 ya kauli hiyo watu walitawanyika na kurudi siku iliyofuta kumzika boda boda
 huyo.
Katika mazishi hayo kuliibuka mambo kadhaa ambapo miongoni mwa mambo 

hayo ni mashekhe wote wa kata ya kichanga kugoma kwenda kumsalia marehmu 
huyo wakiitaka familia hiyo kwenda kumwita mganga huyo wa kiennyeji 
wanayemuami aje kumsalia marehemu wao.


Familia hiyo baada ya kuona viongozi hao wa dini wamevuta 'Hend Breck' 

wameamu kukodi boda boda na kwenda kumfuata shekh Mageta ambaye ana 
undugu na familia hiyo na kwamba kwenye mawaidha yake Shekh Mageta akiipiga 
madongo familia hiyo kwa kuabudu mambo ya kishirikina.


"Nimepata habari mashekh wenzangu wa eneo hili wamesusia kuja 

kwenye msiba huu kwa mambo yetu ya kijinga ya kuabudu ushirikina kijana 
wetu amekufa kwa ajari na ameangukia kichwa damu nyingi zimetoka leo 
mnaenda kuangua kwa mganga kuchunguza kifo chake na mnadanganywa 
eti mganga huyo naweza kumfufua mtu mbona ameshindwa kumfufua naomba
siku nyingine msiludie jambo hili" alisema Shekhe mageta kwenye mawaidha yake.
Mwenyekiti wa mtaa huo wa chuma Bw Nathanael Chacha ambaye alikiri 

kupokea taarifa za familia hiyo kumfufua kijana wao alijaribu kuwaambia 
wajumbe wake waliokuwa kwenye zoezi la kuchanga pesa za pole kuacha 
zoezi hilo.
Jambo la tatu lililojiri kwenye msiba huo ni kwamba kwenye akaunti ya simu

 ya marehemu kulikutwa pesa taslimu shilingi laki sita na kwamba dada za 
marehmu walihangaika kuzitoa pesa hizo bila mafanikio baada ya kushindwa 
kuitambua namba ya siri ya marehmu huyo licha ya kujari kuweka namba ya 
siri ya mwaka wa kuzaliwa wa maremu huyo.
Baba mzaza wa marembu Mzee Abed Shabani alipohojiwa na mtandao huu 

alikiri simu ya mwanae huyo kuwa na kiasi hicho cha fedha na kudai kwamba 
wanashindwa kuzitoa baada ya kutoitambua namba ya siri, habari ambazo 
mtandao huu umezinasa zilidai kwamba mchumba wa boda boda huyo ambaye 
amezaa naye mtoto mmoja ndiye pekee anayejua namba za siri za simu ya 
mpenzi wake na kwamba kuna habari zinadai kwamba wifi zake kwa sasa 
wamemficha jambo hilo naye amedai kwamba kamwe hawezi kuwatajia 
namba hizo za siri mpaka atakapohakikishiwa mgao wa fedha hizo kwa yeye na
 mtoto wake.
 
Mwendelezo wa tukio hili kwa picha za mazishi usikose kutemebea mtandao huu 
kujua mengi juu ya tukio hili ikiwemo ya bibi huyo wa marehemu aliyetumia uchawi 
naye kufariki duni kwa Sangoma huyo

Pikipiki yake ikiwa safi haijaaribika popote kama inavyoonekana 

Polisi wakimpakia kwenye gari boda boda huyo kwa lengo la kumpeleka 

hospitali ambapo kabla ya kufika hospitali boda boda huyo alifia njiani.





Mungu ni mkubwa dereva wa baiskeli hiyo alimpakia mwanae ambaye 

hakuumia popote kwenye ajari hiyo

Gari ya polisi ikielekea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.

No comments:

Post a Comment